Pre GE2025 Huenda huu ukawa ndio mwanzo wa mwisho wa Siasa za Peter Msigwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Inawezekana kuwa ndio mwisho wa CHADEMA kama chama cha kwanza cha upinzani kama Msigwa atafukuzwa chama. Sidhani kama hili watalifanya, kwa vile CHADEMA inaelewa kuwa Msigwa ni JEMBE.
Huwezi kushindana na taasisi yoyote ukaishinda.
Unachoweza ni kuiacha taasisi au ukubaliane nayo.
Hakuna mtu mkubwa kuliko taasisi.
 
Mchungaji Msigwa kubali yaishe. Ubunge wa Iringa Mjini 2025 ni wako kupitia CHADEMA. Wasikudanganye ule upande mwingine kwa kukuhaidi kuwa Mkuu wa Wilaya.
 
CCM Kuna njia nyingi ambazo Msigwa anaweza kupita na kuwa mbunge. Mojawapo ni zile nafasi 10 za mwenyekiti wa ccm taifa a.k.a rais wa JMT. Kama Mbowe anazingua,. Msigwa ahame aingie ccm ambako atateuliwa kuwa mbunge Kisha waziri wa katiba na sheria na ndipo ataifuta chadema kupitia msajii wa vyama vya siasa.
 
Mchungaji kaza haiwezekani Mtu aongoze taasisi miaka 30
 
Huwezi kushindana na taasisi yoyote ukaishinda.
Unachoweza ni kuiacha taasisi au ukubaliane nayo.
Hakuna mtu mkubwa kuliko taasisi.
Siongelei mtu,nami si mwanachama wa chama chochote.
Lakini ni ngumu mtu kuishinda taasisi aliyomo.
Iwe Kanisa,Chama cha Siasa,Kampuni etc.
Anachoweza ni kukaa kando au kukubaliana nayo.
Mmmmmm! KANU kama taasisi ilipotea baada ya Majembe kujitoa. CUF vile vile, NCCR Mageuzi nayo ilipitia njia hiyo hiyo. The next ni ANC, Kuondoka kwa Zuma ni janga kwa ANC. The Zuma efect imeipunguzia ANC 15% ya kura.
Pengine hujui nguvu ya Msigwa katika mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya. Kwa mtafaruku huu tu, Sugu anajua kuwa hana ubunge Mbeya lakini Msigwa ana uhakika wa 100% ya kurudi bungeni. Yahifadhi maneno yangu.
 
Wakuu Mfumo demokrasia ni nzuri kwa wanasiasa inapowapa nafasi lakini ikiwakataa wanaikana.

Miaka kumi ya msigwa kanda ilitosha kwa msigwa kufanya mabadiliko ya muda wa madaraka ya chama.

Sasa bahati mbaya mwenzake kamshinda na hajui lini ataaachia madaraka maana hakuna ukomo huko Chadema.

Na Mbowe alivomjanja anaweza kuruhusu marudio na ukashindwa pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…