Pre GE2025 Huenda Kamati kuu hii ya CHADEMA ikawa ndio mwanzo wa mwisho wa nguvu za Freeman Mbowe au Mwanzo wa Vita mpya ya wazi kati yake na Tundu Lissu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hawa lazima wapasuane Kila mmoja anataka asili nyingi iwe yake.
Tanzania hakuna Upinzani
Upinzani utatoka CCM TU
Ninakumbuka wakati Chadema inapitishwa kwenye mapito yake CCM walisema na kutuaminisha Chadema ya Wachaga upepo ukapita, wakasema ya kasikazini upepo ukapita, wakasema ya wakristo ingawa nakumbuka kuna kipindi Mkapa alikuwa mwenyekiti, Mangula, Jackson Msome nk hatukusema CCM ni ya kikristo. Ukafika muda baada ya tukio moja nakumbuka Arusha wakasema Chadema imejilipua oh ni ya kigaidi. Sasa hv wanatengeneza lugha mpya eti tukate tamaa. HATUKATI. Mti wenye matunda ndo unaopigwa mawe. Haujiulizi vyama vingine vipo c wavishambulie hivyo?
 
Mtasema yote
 
chadema sasahivi kuna tatizo ila chawa wa chadema hawataki kukubali tu hivi kam amakamu anamwambia mwenyekiti kala rushwa kuna nini tena hapo unamvua nguo mwenyekiti yaani lissu hana adabu hata kidogo sasa na wale walikuwaga wanaongea kama watu safi kweli kina heche nao wala rushwa jamani halafu mnataka kushika dola kwa majaribio kweli are you serious chadema?
 
heheee mwenyekiti kalamba rushwa na wengine wenye nguvu wamelamba rushwa bado unajisifu mna chama chenye viongozi wasafi hapo?
 
Aiseee ni hatari sana, Kumbe mpaka Heche yumo?
 
Wakati unaendelea na kuwananga chadema!!?hoja zake mmezijibu!!?

Katiba imepatikana!?

Maana katiba mpya siyo ajenda alioianzisha chadema Bali ni sisi CCM na fedha za walipa Kodi tukala na katiba Hadi leo haijapatikana!!

Tuache uhuni tujitathmini sisi kama sisi tunatosha Kwa wananchi!!?au tusubiri mbeleko ya Dola na jeshi la polisi!!?

Tujibu hoja zake za Muungano na Katiba mpya tuache uhuni was kuwananga wapinzani!!
 
Achana na katiba kama ni majizi hata mkipewa Katiba bado ni majizi tu
 
Achana na katiba kama ni majizi hata mkipewa Katiba bado ni majizi tu
Majizi yapi!!?sisi ccm Kwa mujibu was ripoti ya CAG kaitaja chadema!!?

Cage report imemtaja nani!?kama sio office zetu za seriakali yetu!!?

Chadema Ina Dola!!?kati ya ccm na chadema nani anamiliki dola!!?
 
Tuupe muda muda tuone.

CHADEMA ni chama huru kuweka fikra zako mezani zikajadiliwa na kisha kukubaliana kutofautiana muafaka ukakubalika.

Tofauti na chama kongwe dola ambacho hadi fomu ni moja tu inatolewa kwa kuogopa hoja kizani zikajadiliwa na kukubaliana kutofautiana kisha chama kinakaendelea baada ya muafaka.
 
Fisi endelea kusubiri mkono udondoke,jambo ambalo halitakaa litokee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…