Pre GE2025 Huenda Kamati kuu hii ya CHADEMA ikawa ndio mwanzo wa mwisho wa nguvu za Freeman Mbowe au Mwanzo wa Vita mpya ya wazi kati yake na Tundu Lissu

Pre GE2025 Huenda Kamati kuu hii ya CHADEMA ikawa ndio mwanzo wa mwisho wa nguvu za Freeman Mbowe au Mwanzo wa Vita mpya ya wazi kati yake na Tundu Lissu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Abrams

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2024
Posts
276
Reaction score
338

Wakati Tundu Lissu akiwa anaamini mwenyekiti wake Bw Freeman Aikael Mbowe analamba asali toka Kijiji Cha Nyuki kilichopo huko Singida,

Tayari Kuna taarifa za chini chini kuwa asali pia inalambwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati kuu ambao mara nyingi wamejitanabaisha kama vijana imara na watu wasiopenda rushwa wala Ufisadi.

Wakati Freeman Aikael Mbowe anashambuliwa kulamba asali taarifa zisizo rasmi yeye anatumia mwanya wa Tundu Lissu kumnanga Rais Samia hasa kualikwa na BAWACHA kama silaha ya kumdhoofisha katika hoja yake hiyo ya kulamba asali.

Kabla ya Kamati kuu hii ni Tundu Lissu pamoja na John Heche ndio walionekana kuwa na nguvu ya kutwaa nafasi ya Uenyekiti wa Taifa hasa baada ya Freeman Mbowe kudhoofishwa na hoja ya Ulambaji wa asali.

Huenda Freeman Aikael Mbowe akairejesha nguvu yake hasa baada ya kumbana Tundu Lissu kwenye hoja zake za kuropoka ropoka ikiwemo hoja yake ya kutaka kuligawa Taifa la Tanzania.

Tundu LIssu, Freeman Mbowe na John Heche ndio wanachama wanaopewa nafasi kubwa ya kuiongoza CHADEMA kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Ule Uchaguzi Mkuu wa Mwakani.

Je, Baada ya yote CHADEMA kutoka salama au tutarajie CHADEMA kutoka vipande vipande kama ilivyokuwa kwa NCCR, CUF na hata TLP?

#Tuupe muda muda tuone.

 

Wakati Lissu anaamini mwenyekiti wake Bw Freeman Aikael Mbowe analamba asali toka Kijiji Cha Nyuki kilichopo huko Singida,

Tayari Kuna taarifa za chini chini kuwa asali pia inalambwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati kuu ambao mara nyingi wamejitanabaisha kama vijana imara na watu wasiopenda rushwa Wala Ufisadi.

Wakati Mbowe anashambuliwa kulamba asali taarifa zisizo rasmi yeye anatumia gape la Lissu kumnanga Rais Samia hasa kualikwa na BAWACHA kama silaha ya kumdhoofisha katika hoja yake hiyo ya kulamba asali.

Kabla ya Kamati kuu hii ni Lissu pamoja na John Heche ndio walionekana kuwa na nguvu ya kutwaa nafasi ya Uenyekiti wa Taifa hasa baada ya Mbowe kudhoofishwa na hoja ya Ulambaji wa asali.

Huenda Mbowe akairejesha nguvu yake hasa baada ya kumbana Lissu kwenye hoja zake za kuropoka ropoka hasa kwa hoja yake mbaya ya kutaka kuligawa Taifa la Tanzania.

LIssu, Mbowe na Heche ndio wanachama wanaopewa nafasi kubwa ya kuiongoza CHADEMA kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Ule Uchaguzi Mkuu wa Mwakani.

Je, Baada ya yote CHADEMA kutoka salama au tutarajie kutoka vipande vipande?

#Tuupe muda muda tuone.

Stupid necked fools
 
Nadhani Mods waweke utaratibu mzuri ili waliojiunga humu chini ya mwaka mmoja wawe wasomaji tu!! Hii hatua itasaidia kuwachuja CHAWA ambao kwa hivi karibuni wamemwagwa humu kwa wingi. Sasa kama huyo mwenye wiki tatu naye analeta mada!!? No
Sasa humu tunajadili "mada" au "mleta mada",

CHADEMA mbona uelewa wenu uko chini sana?
 
Nadhani Mods waweke utaratibu mzuri ili waliojiunga humu chini ya mwaka mmoja wawe wasomaji tu!! Hii hatua itasaidia kuwachuja CHAWA ambao kwa hivi karibuni wamemwagwa humu kwa wingi. Sasa kama huyo mwenye wiki tatu naye analeta mada!!? No
Halafu hawana hata adabu wanatukana tukana hovyo
 
Boni tunasikia na wewe umevuta mzigo ukajenga hekalu halafu unatuambia ni "Kitu ya yai" 🤣🤣🤣🤣
Joined 27 April 2024, sasa mnapojiunga someni sheria za JF, Zinakataza kutaja majina ya watu humu jf, kibaya zaidi wewe unataja uongo
 
Joined 27 April 2024, sasa mnapojiunga someni sheria za JF, Zinakataza kutaja majina ya watu humu jf, kibaya zaidi wewe unataja uongo
Boni ndio nani?
Yai ndio nini?

Kuwa serious BAVICHA.
 
Back
Top Bottom