Wakati Tundu Lissu akiwa anaamini mwenyekiti wake Bw Freeman Aikael Mbowe analamba asali toka Kijiji Cha Nyuki kilichopo huko Singida,
Tayari Kuna taarifa za chini chini kuwa asali pia inalambwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati kuu ambao mara nyingi wamejitanabaisha kama vijana imara na watu wasiopenda rushwa wala Ufisadi.
Wakati Freeman Aikael Mbowe anashambuliwa kulamba asali taarifa zisizo rasmi yeye anatumia mwanya wa Tundu Lissu kumnanga Rais Samia hasa kualikwa na BAWACHA kama silaha ya kumdhoofisha katika hoja yake hiyo ya kulamba asali.
Kabla ya Kamati kuu hii ni Tundu Lissu pamoja na John Heche ndio walionekana kuwa na nguvu ya kutwaa nafasi ya Uenyekiti wa Taifa hasa baada ya Freeman Mbowe kudhoofishwa na hoja ya Ulambaji wa asali.
Huenda Freeman Aikael Mbowe akairejesha nguvu yake hasa baada ya kumbana Tundu Lissu kwenye hoja zake za kuropoka ropoka ikiwemo hoja yake ya kutaka kuligawa Taifa la Tanzania.
Tundu LIssu, Freeman Mbowe na John Heche ndio wanachama wanaopewa nafasi kubwa ya kuiongoza CHADEMA kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Ule Uchaguzi Mkuu wa Mwakani.
Je, Baada ya yote CHADEMA kutoka salama au tutarajie CHADEMA kutoka vipande vipande kama ilivyokuwa kwa NCCR, CUF na hata TLP?
#Tuupe muda muda tuone.