Huenda kosa lingine ni kuteua na kuchukua darasa la saba wengi kwenye majeshi

Huenda kosa lingine ni kuteua na kuchukua darasa la saba wengi kwenye majeshi

Prof Koboko

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
350
Reaction score
2,550
Siamini kabisa mambo yanayofanywa na polisi wetu kama kuna weledi wowote wa kiufundi unaozingatia taaluma zao. Naona kabisa shida kubwa zamani tukikosa wasomi recruitment ikawa inachukua darasa la 7 na huenda hawa ndio Ma-RPCs na OCDs wengi na baadhi ya Waandamizi pale HQ. Hii ndio shida mojawapo. Kumkuta Askari ana shule huwezi kumkuta ngazi za juu, utakuta kwenye vitengo viingine vidogo vidogo tu. Hawa wanasumbua ni wazee wetu wa zamani wanaojiendeleza wenye diploma,degree kidogo na wengine hawana kabisa.

Kama ni mabadiliko ya kuajiri wasomi ndani ya majeshi ni awamu ya JK kuanzia 2006 hapa mpaka sasa na ndio maana wasomi wengi ndani ya majeshi yetu ni vijana chini ya miaka 45. Hawa wengi hawana nafasi kwenye maamuzi wapo kwenye units ndogo ndogo tu. Kuna haja ya Reformation kwenye majeshi yetu kama kweli tuna nia njema na taifa letu. Sisi tuliokulia kulia kwenye familia hizi tunaelewa vizuri ingawa mimi binafsi sikupenda kuingia huko.

Haiwezekani leo polisi waziri unaagizwa na waziri kwa jambo ambalo ni senstive bkabisa kwenye usalama wa nchi unajibu mpaka upewe barua lakini Ma-RPCs na OCDs huko wanakamata watu na kujaza mahabusu tu kisa Wanadai Katiba mpya. Haiwezekani leo Polisi unasema Flani ana kesi ya kupanga njama za kuua viongozi wa juu wa serikali lakini kesho yake kwenye hati ya mashtaka haipo, huku ni kukosa weledi na kwa fikra zangu ndio hawa wa recruitments za Mkapa na Mwingi ndio wako kwenye maamuzi,siamini kama vijana ambao ni wasomi wazuri wanaweza kufanya mambo haya.

Mama Samia Amir Jeshi wetu mkuu, tunakuomba sana fanyika mabadiliko jeshi la polisi ikizingatiwa wamebeba Unitis muhimu kama ya Upelelezi na huenda ndio sababu ya mahabusu kujaa nchini, hizi kesi za kubambikiza chanzo ni hili kundi. Upelelezi unahitaji uwezo mkubwa wa akili, wanahitajika vijana weledi wenye degree za Sheria, sayansi ya jamii, saikolojia nk. Kama kweli tuna lengo la kuboresha basi tufanyie kazi huu ushauri.
 
Back
Top Bottom