Huenda ' Mikosi ' ya Yanga SC kufanya vibaya huwa inaanzia kutoka kwa hawa Wasemaji wake wa ' hovyo hovyo ' Bumbuli na Nugaz

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Leo asubuhi akihojiwa na Wasafi FM kupitia Mtangazaji Yussuf Mkule Msemaji wa Yanga ya Mshindo Msolla aitwae Hassan Bumbuli kwa ' Majigambo ' kabisa alisema kuwa Yanga imepanga Kufanya ' Mauwaji ya Shalubela ' kuliko yale yaliyofanywa na Simba SC na Azam FC ya Kuifunga Singida United Goli 8 alizoshinda Simba na Goli 7 alizoshinda Azam. Cha Kushangaza baada ya Mechi leo Yanga Kamfunga Singida United Goli 3 tu kwa 1.

Leo asubuhi akihojiwa na Efm kupitia Mtangazaji Mwanadada Tunu Hassan Shemkome Msemaji wa Yanga ya GSM aitwae Antonio Nugaz kwa ' Majigambo ' kabisa alisema kuwa Yanga imepanga Kufanya ' Mauwaji ya Halaiki ' kuliko yale yaliyofanywa na Simba SC na Azam FC ya Kuifunga Singida United Goli 8 alizoshinda Simba na Goli 7 alizoshinda Azam. Cha Kushangaza baada ya Mechi leo Yanga Kamfunga Singida United Goli 3 tu kwa 1

Hivi kama Klabu tu inakuwa na Wasemaji ' Wapuuzi ' kama hawa Wawili unategemea akina Molinga Watafunga na akina Morisson Kutowasusia?
 

Kimfaacho mtu chake, kipigo kiliwafaa
 
Mchezaji mwanye akili hawezi baki utopolon kwasababu kuanzia viongoz mpaka mashabiki lia lia hawajielewi akili zao zimejaa makando kando na lawama yanga hata aje mchezaj mzur VP hawez kaa kwenye club iliyo jenga misingi kwenye lawama badala ya vitendo
 
Simba na Yanga wote wanawasema hovyo sana. Lakini yanga wanasemaji hovyo zaidi. Timu zetu hazina mikakati ya mafanikio kimataifa zaidi ya kuwapumbaza mashabiki wao kwa kauli za hivyohivyo km hizo za wakina Nugaz. Timu za Tanzania hazina wasemaji wenye kujitambua mara zote n tambo za kuifunga yanga au Simba tu.
 
Kwani Yanga ina wasemaji wangapi na kanuni kuhusu idadi ya wasemaji wa klabu inasemaje
 
Hahahaha Sijui Kama ni wapuuzi au vipi....ila kauli yako imenichekesha Sana...uko sahihi kwa namna Fulani...wanamuiga msemaji was timu Fulani...very hopeless...they are amateurs...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…