Huenda mwanamama aliyeteka hisia ya wengi aliingia mtego wa matapeli wanaotuma SMS za kiganga

craq

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
859
Reaction score
1,866
Hot news iliyopo sasa ni tukio la mwanamama aliyeshindwa kuhimili pressure na misukosuko hivyo aliamua kwenda kwa mganga ili amsaidie nyumba waliyokuwa wanaishi isipigwe mnada.

*Awali ya yote nina wasiwasi huenda mwanamama yule aliingia mtego tu kwa mashuhuda wanasema yule mama alikuwa anaongea na simu wakati anaratibu tukio huko ukonga.Kweli mganga anatoa maelekezo kupitia simu?

Kuna mchezo umezuka ya message kutumwa na watu wasiojulikana wakijidai ni waganga wenye uwezo wa kutoa mikosi ,kutoa utajiri na ukipatwa tamaa ukiwatafuta wanakuambia uwatumie hela ,majina 3 na shida kisha wanakupa maelekezo ya uongo kisha inakula kwako naamini wengi wameshakutana na messages hizi kwenye simu,huenda mwanamama huyu wakati yupo na stress,mawazo alitumiwa SMS hii na kutokana na shida na panic akaingia kwenye mtego wa matapeli wale ndio maana akawa anapewa maelekezo feki kupitia simu

Nina wasiwasi huyu mama aliingia kwenye mtego tu ya sms ya utapeli wa waganga feki .

Na kama kweli alienda kwa mganga basi mganga yule aliona mbali ,huyu jamaa huenda akapata huruma ya wananchi na TRA maana hili suala imewagusa wengi na akahurumiwa.
 
Aende kwa Yesu Kristu akiwa na imani, kila ana choomba atafanikiwa.Tena ni bure
 
Kumbe una wasiwasi...hata mimi nina wasiwasi na hii habari yako
 
Hii ni hot news ndani ya familia yako au hapo kijiweni kwenu tu!! Unamwongelea mtu ambaye hakuna anayemjua wala kumsikia wala tukio lenyewe! Halafu unaiita eti hot news! Ptuuu
 
Kipi kinakupa wasiwasi?kwamba yule si mshirikina?kwa vigezo vipi?yule ni mshirikina kama washirikina wengine hao washirikina wenzake kaonana nao uso kwa uso na ndio maana wakampa na vifaa na nguo maalum.
Chawi tu lile kama chawi linginelo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…