Huenda Ruth Zaipuna ndiye Waziri wa Fedha ajaye!

Huenda Ruth Zaipuna ndiye Waziri wa Fedha ajaye!

Wabongo wakiamua kuhype mambo. Ni utendaji gani wa kutukuka husifiwa huyu sisteri?
 
Inawezekana. Maana hiyo NMB Ina mashabiki wengi sana siku hizi, hata viongozi wakubwa ndani ya Mfumo ni wateja wakubwa wa NMB. Nimewahi kumshuhudia Mzee J.K akienda zake NMB Tawi la Mlimani. Sio Mzee J.K tu, hata Jaffo. Kwanini wasitumie benki yao ya serikali ya T.C.B ?!

Hii inadhihirisha kuwa Mama Zaipuna anafanya kazi nzuri na watu wanavutiwa na benki yake kila leo.

Ila mleta mada baada ya huu uzi naamini umeshamuharibia Mama Ruth zaipuna, hatateuliwa tena. Mkijua vitu mkaage kimya! Mnawaharibia wenzenu.
 
Kwa Sasa ndiye Afisa Mtendaji mkuu wa NMB

Benki yenye Mafanikio makubwa sana

Amekuwa akisifiwa sana na Rais Samia Kwa Utendaji Wake Uliotukuka

Sabato njema 😃

Kwako Lucas Mwashambwa
Ni mjinga tu anaweza kuacha nafasi yenye security of tenure kwenda nafasi ambayo mteuaji mwenyewe hawezi kuwa guarantor. Simshauri aingie mtego huo.
 
Imeshawatokea the likes of Maharage Chande, Waziri Kindamba, Zuhura Yunus, Tido Mhando, Kairuki wa TIC.
 
Kukamua mishahara ya wafanyakazi ni kazi rahisi, kuliko kuendesha uchumi wa nchi.

Wajaribu waone, ndio aelewe kazi ya kutunga uongo serikali ipo vizuri wakati mambo ni vulu-vulu kama ni rahisi.

Kuendesha banks za Tanzania ni shughuli nyepesi, uhitaji creativity yoyote na wala kuchukua hata moderate risks.

Unachohutaji ni kufanya biashara na serikali kukwamua sehemu ya tsh 700 kwa mwezi ya mishahara wanayotoa kwa wafanyakazi. Kutumia savings zao kuwakopesha wao wenyewe kupitia bonds na nyingine kidogo kukopeshea biashara.

Vinginevyo hakuna la maana wanalofanya ndio maana kasi ya ukuaji wa viwanda ni ndogo Tanzania. Sehemu kubwa ya shughuli za bank ni biashara na serikali.

Ndio maana Magufuli alikuwa nuksi kwao, jamaa angeinyoosha Tanzania.
 
Back
Top Bottom