Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Bado haijabainika wala haijawekwa wazi kwamba ni sehemu gani ya katiba, sheria au kanuni za uchaguzi zilizokiukwa, lakini tayari mchakato wa kumuita na kumpeleka mbele ya kamati mahususi juu ya mambo haya umekamilika.
Hofu kubwa imetanda kwenye kambi yake na wanasheria wamejipanga vilivyo kumsaidia japo sijui kama inahiusika au itasaidia chochote, kumnasua kwenye mkwamo huo wa kimaadili, ambao unafanana kabisa na ule ambao umemkumba mwenyekiti wa Chadema mkoa wa shinyanga.
Kama mdau wa siasa za Chadema, unadhani Tundu Lisu anaweza kuchomoka kwenye kibano au kikaango hiki cha kimaadili na kisheria na akavuka mchujo wa kugombea uenyekiti wa Chadema Taifa?
Unadhani ni kitu gani hasa kinaweza kumfanya akawajibishwa na chama kimaadili kama alivyowajibishwa mwenyekiti wa Chadema mkoa wa shinyanga?🐒
Mungu Ibarki Tanzania