Kurunzi
Platinum Member
- Jul 31, 2009
- 10,198
- 11,630
Binafsi Nimeshuhudia mambo hovyo kabisa kwenye uchaguzi wa 29/10/2025 Kwa masikitiko, hali ni mbaya zaidi kuliko tulivyoweza kudhani. Nilishuhudia kwa macho yangu jinsi baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi walivyokuwa wakipokea maelekezo ya wazi ya kuhakisha Mama Samia anashinda kwa kishindo Katika vituo vingi, tuliona udanganyifu ukiendelea kwa namna ya ajabu.
Wasimamizi wa vituo walipewa maelekezo kujaza vitabu kwa kumpigia Mama samia Ni wazi kwamba maelekezo hayo yalitolewa ili kufanikisha udanganyifu katika uchaguzi huu.
Maafisa wengi wa uchaguzi walinieleza wazi kuwa walikuwa wamepewa maelekezo ya kuhakikisha ushindi wa Mama Samia, licha ya kuwa hali hii ni kinyume na taratibu na sheria za uchaguzi zilizowekwa na Tume ya Uchaguzi.
Uchaguzi wa mwaka huu umejaa upungufu mkubwa wa uwazi na uadilifu. Wengi wanasema kuwa uchaguzi huu ni mbaya zaidi kuliko ule wa miaka ya nyuma, na kuna hofu kuwa haki ya wananchi kuchagua viongozi wao kwa njia ya haki inaweza kupotea kabisa.
Tume ya Uchaguzi lazima ichukue hatua za haraka ili kuhakikisha kuwa matokeo hayaonyeshi tu mapenzi ya watu, bali pia yanaheshimu sheria na taratibu za uchaguzi.
Tuna jukumu la kulinda demokrasia yetu, na tunapaswa kuungana ili kupigania haki yetu ya kuchagua kwa njia iliyo wazi na ya haki.
Na haya yatawezekana tu ikiwa titapata katiba mpya tofauti na hapo hakuna bora tusipoteze fedha kwa uchaguzi wa kiini macho