Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,386
- 2,833
Kuna mabadiliko mapya yanayoweza kubadilisha kabisa namna tunavyolipia huduma ndani ya Android apps! 🔥
Google inakuja na Mfumo unaitwa Usage-Based Billing ambapo unaruhusu watumiaji kuweza kulipia huduma kulingana na matumizi yao badala ya kulazimika kulipa subscription ya kila mwezi.
Hii ina maana kwamba gharama unayolipa inaweza kutegemea ni mara ngapi umetumia huduma fulani, umetumia kiasi gani cha rasilimali au umefanya shughuli ngapi ndani ya app.
Mfano ikiwa umetumia AI app inayotengeneza video. Badala ya kulipia TSh 30,000 kila mwezi, unaweza kulipia credits kulingana na idadi au ubora wa video unazotengeneza.
Je, Tanzania 🇹🇿 tutapata lini?
Kwa ratiba rasmi ya Google, baadhi ya mabadiliko ya mfumo wa Google Play yanafika katika masoko mengine duniani ifikapo Septemba 30, 2027 Tanzania ikiwemo.
Unaonaje kuhusu mabadiliko haya Mapya tuachie maoni yako ✍️.