Huenda ukaanza kulipia app kwenye Android yako kwa jinsi unavyotumia

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,386
Reaction score
2,833


Kuna mabadiliko mapya yanayoweza kubadilisha kabisa namna tunavyolipia huduma ndani ya Android apps! πŸ”₯

Google inakuja na Mfumo unaitwa Usage-Based Billing ambapo unaruhusu watumiaji kuweza kulipia huduma kulingana na matumizi yao badala ya kulazimika kulipa subscription ya kila mwezi.



Hii ina maana kwamba gharama unayolipa inaweza kutegemea ni mara ngapi umetumia huduma fulani, umetumia kiasi gani cha rasilimali au umefanya shughuli ngapi ndani ya app.



Mfano ikiwa umetumia AI app inayotengeneza video. Badala ya kulipia TSh 30,000 kila mwezi, unaweza kulipia credits kulingana na idadi au ubora wa video unazotengeneza.

Je, Tanzania πŸ‡ΉπŸ‡Ώ tutapata lini?
Kwa ratiba rasmi ya Google, baadhi ya mabadiliko ya mfumo wa Google Play yanafika katika masoko mengine duniani ifikapo Septemba 30, 2027 Tanzania ikiwemo.

Unaonaje kuhusu mabadiliko haya Mapya tuachie maoni yako ✍️.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…