SUBMAC
Member
- Apr 12, 2024
- 11
- 11
Amani iwe nanyi!
Kwa ufupi tu, nimejaribu kuwaza jinsi tabaka hili la watu maarufu, wakiwemo wasanii, linavyoishi kwa kututegemea sisi wananchi na kodi zetu.
Msanii akiwa ana-rise to fame, ataomba support ya mashabiki (sisi) na hata serikali (kupitia mamlaka zinazowahusu) ili afike anapokusudia. Hapo ametumia kodi zetu
Msanii/mtu maarufu anapo-gain momentum, ana-side na serikali kupata madili. Mfano mdogo ni katika shughuli za kiserikali na kisiasa, maarufu hawa hulipwa fedha nzuri kwa kutumbuiza. Ni kodi zetu hizo.
Msanii huyu anapogombana na mwenzake au kutofautiana na upande mwingine, katika harakati za kutetea/kulinda interests zake, huwa mwepesi kukimbilia huruma ya serikali.
Mfano mmojawapo ni ‘bifu’ la Diamond Platnumz na Harmonize ambapo Kondeboy alimpigia simu moja kwa moja Rais Magufuli ili apate huruma yake, maana yake akimuomba kiongozi huyo mkubwa atumie mamlaka yake kuu kushinikiza mambo yaende upande wake yeye Kondeboy.
Msanii ama mtu maarufu anapopata tatizo kubwa hasa la kiafya, huwa mwepesi kutuchangisha wananchi na hata kuiomba Serikali moja kwa moja ichangie i.e. matibabu yake, nk. Mfano mzuri ni mwanahiphop Joseph Haule a.k.a Profesa Jay.
Licha ya utajiri alioingiza kupitia muziki na siasa, bado alihitaji wananchi na serikali isaidie ustawi wake kiafya ilihali kuna pengine mamia (sio takwimu rasmi) ya wagonjwa kama yeye walipoteza maisha yao kwa kukosa msaada ambao serikali ilimpatia Prof Jay, na serikali hiyohiyo ikiwepo. Usanii au umaarufu hapa umekuwa “priveledge”
Suala la mtu maarufu ni ajenda kwa kiongozi au mwanasiasa. Ishu kama ya Feitoto zipo nyingi mitaani (japo sio katika muktadha wa soka), lakini huenda hazijapata hata usuluhishi kwa baraka ya uongozi tena wa juu kama ilivyo kwake Feitoto.
Hayo ni miongoni tu mwa mengi yanayonishawishi nifikiri kuwa “these privileged individuals might be the most silent beggars”
Unaweza kuongeza mifano na justifications.
Alamsiki!