Judi mama wa hekima,bila hiana shauri,
Kijana mwama wandima,ahitaji si kidari,
atakwenda hata kupima,iwapo kipo kigori,
Heri mwana wewe heri,mpate aliye kimwana,
Sina mengi kwa hilo,mora akupe nguvu,
ushauri kwetu ulo,umpate wako ubavu,
hata kama nyalukolo,wala isiwe mabavu,
heri mwana wewe heri,mpate aliye kimwana,
wapi ulipotelea, ewe nguli wa vina,
vipi umeingilia, tena wanena kichina,
wenzio tunaringia, ugha adhimu jichana
wandima anabugia, eti bora msichana
wapi ulipotelea, ewe nguli wa vina,
vipi umeingilia, tena wanena kichina,
wenzio tunaringia, ugha adhimu jichana
wandima anabugia, eti bora msichana
Nimekubali,
we mkali,
umeshuka mashairi,
utadhani huna akili,
pongezi wastahili, lol
wapi ulipotelea, ewe nguli wa vina,
vipi umeingilia, tena wanena kichina,
wenzio tunaringia, lugha adhimu jichana
wandima anabugia, sasa asaka msichana
Umenikoti vibaya, sikuwahi sema hivyo,
Ningeokota malaya, kama ingekuwa ndivyo,
Eti bora msichana, ntakuwa mtu wa hovyo
Penzilo nishalikosa, nimevikosa vigezo,
Kwa mbali ukanitosa, nshajiona hamnazo,
Kama yuko wa kunikosha, ajitoe kimasomaso.
Bora eti msichana, na msichana si bora,
wandima taka jichana,pasipo angalia ubora,
niko mama nahakana,kutaka yangu mi bora,
Mwacheni atake bora,si bora ije mtake,
Kuwakoseni ni haki,jukwaa lililo mwake,
swala lisilo mkiki,la kuoa uwe wake,
wandima si mhakiki,judi magu tuwe nake,
Mwacheni atake bora,si bora ije mtake,
Nakipenda chetu lugha,kiswa kina uhamsu,
wala sija kuwa juha,walahi hata kwa busu,
hutamka hata waha,usukuma mpaka lisu,
Macheni atake bora,si bora ije mtake,
ni nini kimekusibu, mbona waruka kimanga,Umenikoti vibaya, sikuwahi sema hivyo,
Ningeokota malaya, kama ingekuwa ndivyo,
Eti bora msichana, ntakuwa mtu wa hovyo
Penzilo nishalikosa, nimevikosa vigezo,
Kwa mbali ukanitosa, nshajiona hamnazo,
Kama yuko wa kunikosha, ajitoe kimasomaso.
ni nini kimekusibu, mbona waruka kimanga,
na judi wanisulubu, sababu zako wachonga,
vipi ugeuke bubu, shindwe hata kulonga,
na judi si mwarabu, hawezi hata kuringa?