Ms Judith
JF-Expert Member
- Dec 24, 2010
- 2,563
- 929
Judi mama wa hekima,bila hiana shauri,
Kijana mwama wandima,ahitaji si kidari,
atakwenda hata kupima,iwapo kipo kigori,
Heri mwana wewe heri,mpate aliye kimwana,
Sina mengi kwa hilo,mora akupe nguvu,
ushauri kwetu ulo,umpate wako ubavu,
hata kama nyalukolo,wala isiwe mabavu,
heri mwana wewe heri,mpate aliye kimwana,
wapi ulipotelea, ewe nguli wa vina,
vipi umeingilia, tena wanena kichina,
wenzio tunaringia, lugha adhimu jichana
wandima anabugia, sasa asaka msichana