Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Hugo Rafael Chaves Frias alizaliwa 28 July 1954 na alifariki 05 March 2013. Alikuwa mwanasiasa wa Venezuea ambae aliitumikia nchi yake kama rais wa 64 wa nchi hiyo kutoka mwaka 1999 mpaka 2013. Alikuwa kiongozi wa Fifth Republic Movement kutoka kuanzishwa kwake mwaka 1997 mpaka 2007 kilipoungana na vyama vingine kuunda United Socialist Party of Venezuela (PSUV), na aliongoza chama hicho mpaka 2012.
Alizaliwa katika familia ya watu wa kawaida waliotegemea kipato kwa kufanya kazi katika mji wa Sabaneta, Barinas, Chaves alikuja kuwa ofisa wa jeshi na hakuridhika jinsi wanasiasa wa Venezuela walivyojikita kwenye Punto Fijo Pact, alianzisha kwa siri Revolutionary Bolivarian Movement-200(MBR-200) mwanzoni mwa miaka ya 1980. Chaves aliongoza MBR-200 katika mpango wa kupindua serikali ya Democtratic Action iliyoongozwa na Rais Carlos Andres Perez mnamo 1992, na kwasababu hiyo alifungwa jela.
Alipotoka jela baada ya miaka miwili, alianzisha chama cha siasa kilichojulikana kama Fifth Republic Movement na alichaguliwa kuwa rais wa Venezuela mwaka 1998. Alichaguliwa tena mwaka 2000 na tena mwaka 2006 kwa jumla ya asilimia 60 ya kura zote. Baada ya kushinda mhula wa nne wa urais katika uchaguzi wa mwezi October 2012 ilikuwa aapishwe January 10 2013, lakini Bunge liliairisha sherehe hizo za kuapishwa ili kumpa nafasi ya afya yake kuimarika kutoka kwani alikuwa anatoka kwenye matibabu nchini Cuba. Alisumbuliwa na cancer iliyogundulika June 2011, Chavez alikufa mjini Caracas mnamo tarehe 05 March 2013 akiwa na umri wa miaka 58.
Kufuatia mpangilio wa mfumo 1999, Chaves alilenga katika kuamuru mabadiliko katika huduma za jamii katika Bolivarian Revolution, hii ilikuwa kama sera ya ujamaa. Kutumia tarakimu za mapato ya mafuta miaka ya 2000 serikali yake ilipitisha ushirikiano wa kidemokrasia uliojulikana kama Communal Councils, na hii ilipelekea kuanzishwa kwa mipango ya kijamii iliyojulikana kama Bolovarian Missions iliyopanua upatikanaji wa chakula, nyumba, huduma za afya na elimu. Venezuela ilipata faida kubwa ya mafuta katikati ya miaka ya 2000, na kulikuwa na mabadiliko katika hali duni ya maisha, elimu, uwiano wa kipato na ubora wa maisha kwa ujumla kati ya 2003 na 2007. Kufikia mwisho wa urais wa Chaves mwanzoni mwa 2010, sera za uchumi zilizowekwa na serikali kama kubana matumizi na kudhibiti bei kulidhihirika hakuwezi kuendesha serikali wakati uchumi wa Venezuela ulikuwa unayumba, umasikini, bei za bidhaa zilipanda na mzunguko wa pesa ulipungua. Hii ilipelekea kiwango cha mauaji katika nchi kupanda, rushwa iliendelea katika idara za serikali mpaka polisi. Mfumo wake wa kuwezesha na kujitangaza kweke pia kulileta shida.
Kimataifa, Chavez alijijengea taswira kama mfuata mfumo wa Marxist na Lenini ambao Fidel na Raul Castro wa Cuba waliufuata, pia serikali ya Evo Morales (Bolivia), Rafael Correa (Ecuador) na Daniel Ortega (Nicaragua). Urais wake ulionekana kama ujamaa uliokwenda na wakati "pink tine" uliyosafisha Latin America.
Hugo alieleza sera zake kama za kupinga ubeberu, alionekana kama mtu mashuhuri aliyepinga sera za nje ya nje ya siasa za Marekani kwa sauti na upinzani wa hali ya juu. Aliunga mkono mfumo wa uchumi kumilikiwa na serikali. Alieleza kuwa yeye ni mfuata ujamaa na aliungwa mkuono na Latin American and Carribiean Cooperation, yeye alikuwa dhana ya kuunda umoja wa kanda ya Union of South American for the Americans, Bank of the South na pia television ya TeleSUR. Mawazo haya yalipelekea style ya Chavismo ambayo ni mfumo wa siasa ulioshirikisha Bolivia na ujamaa wa karne ya 21.
Maisha ya awali.
Alizaliwa 28 July, 1954 katika nyumba ya bibi yake mzaa baba Rosa Inez Chaves, ilikuwa nyumba ya kisasa kwa wakati huo, yenye vyumba vitatu vya kulala, ilikuwa katika kijiji cha Sabaneta, Mkoa wa Barinas. Famila ya Chaves ilikuwa ya Wamarekani-Wahindi, Waafrika-Wanezuelan na Waspanish kwa asili. Wazazi wake, Hugo de los Reyes Chaves, anaelezewa kuwa mtu mwenye kujisikia wa jumuia au chama cha Wakristu COPEI, na mama yake Elena Frias de Chaves wazazi wote walikuwa walimu na waliishi katika kijiji kidogo huko Los Rastrojos.
Hugo alikuwa mtoto wa pili katika watoto saba. Hugo analielezea kuwa maisha yake ya utoto yalikuwa ya "kimasikini na yenye furaha", pamoja na kuwa utoto wake uliodhaniwa wa kimasikini ndiyo inajadiliwa ulimsukuma kubadilisha hadithi ya misha yake kuwa ya siasa. Alikwenda shule ya msingi ya Julian Pino, Chavez mwenyewe alipendezewa na mfumo wa serikali moja wa karne ya 19 (federal) ulioongozwa na generali Ezequiel Zamora, babu wa babu yake alikuwa mfanyakazi kwa generali huyo. Hakukuwa na shule ya juu (high school) katika sehemu waliyoishi, wazazi wake walimpeleka Hugo na kaka yake Adan kuish na bibi yao Rosa, ambae aliishi katika nyumba ya watu wenye uwezo wa kati na sehemu ya (kodi) ya nyumba hiyo yalilipwa na serikali. Pale Hugo na kaka yake Adan walikwenda shule ya Daniel O'leary High School, miaka ya 1960. Hugo alimuelezea bibi yake baadae kuwa alikuwa "binadamu kamili mwenye mapenzi na roho nzuri". Bibi yao huyo alikuwa muumini mzuri wa Kikatoliki, na Hugo alikuwa msaidizi wa madhabahuni katika kanisa lao la karibu. Baba yake pamoja na kupata mshahara wa ualimu ilibidi alipe ada ya Chaves na ndugu zake.
Shule ya Kijeshi 1971-1975
Akiwa na miaka 17, Chavez alisoma katika shule ya Venezuelan Academy of Military Science mjini Caraca, kufuatia mfumo wa elimu uliojulikana kama Andres Bello Plan, mfumo huu ulibuniwa kwa watakao endelea na jeshi la taifa kama maofisa wa jeshi. Mfumo huo haukuwafundisha wanafunzi mbinu za kijeshi tu bali pia walijifunza masomo mengine, na kwakufanya hivyo maprofesa waliletwa kutoka katika vyuo vikuu vingine kuwapa mafunzo katika shule hiyo ya kijeshi.
Wakati akiishi Caracas, aliona umasikini usioisha uliowakabili watu hali ya chini na wafanyakazi katika Venezuelea, na alisema mtazamo ule ulimfanya awe na nia ya dhati kufikia malengo ya kubadilisha hali ya jamii. Alianza kujishughulisha na shughuli nje ya jeshi kama kucheza baseball na mpira wa laini pamoja na Criollitos de Venezuela team, maendeleo hayo yalimpelekea kuchezea timu ya taifa. Aliandika mashairi pia kutunga hadith, alicheza ngoma na kuchora, alifanya uchunguzi wa maisha ya siasa yalivyokuwa katika karne ya 19 katika America ya kusini na mapinduzi ya Simon Boliva.
Alianza kuwa mshabiki wa mwanamapinduzi wa Marxi aliyeitwa Che Guevara aliyezaliwa mwaka 1928 na kufariki mwaka 1967 baada ya kusoma kumbukumbu zake 'The Diary of Che Guevara'. Mnamo mwaka 1974 alichaguliwa kuwa mwakilishi katika kumbukumbu ya miaka 150 ya Vita ya Ayacucho Peru, ugomvi ambao luteni wa Simon Boliva aliyeitwa Antonio Jose de Sucre aliyashinda majeshi ya mfalme katika Peruvian War of Independence. Akiwa Peru, Chaves alisikia rais wa mwengo wa kushoto Generali Juan Velasco Alvarado (1910-1977), akiongea, alivutiwa na mwongozo wa Velasco kuwa jeshi liwe msimamizi wa watu wa hali ya chini wakati watu wa juu wakiwa walarushwa wasio waaminifu, "alianza kunywa vitabu vyote vilivyoandikwa na Velasco mpaka kufikia kukariri baadhi ya hotuba". Alianzisha urafiki na mtoto wa Kiongozi wa Marxi Omar Torrijos, diktekta wa mwengo wa kushoto wa Panama, Chavez alitembelea Panama, ambako alikutana na Torrijos, alivutiwa na mfumo wake wa kumiliki ardhi ambao ulikusudia kuwanufaisha wakulima. Kwa ushawishi wa Torrijo na Velasco alianzo kuona uwezekano wa magenerali wa jeshi kuchukua madaraka ya serikali waka uongozi wa wananchi ukikosa uaminifu na kuzama kwenye rushwa ambaya inanufaisha matajiri wachache. Kwa kulinganisha mawazo ya Torrijo na Velasco, Chavez alianza kuwa kumshutumu kwa nguvu Augusto Pinochet ambae alikuwa generali wa mwengo wa kulia aliyejichukulia madaraka ya Chile kwa msaada wa Marekani.
Maisha ya mwanzo kama Mwanajeshi.
Baada yakuhitimu, Chavez alipangiwa kazi kama ofisa wa mawasiliano katika kituo cha chunguza wenye mipango ya kupindua serikali mjini Barinas, pamoja na sera za Marxi na Lenini wapinga serikali ambao jeshi lilitaka kuwafuatilia walishaanza kuondolewa kutoka serikalini. Kuna kipindi alijikuta mkusanyiko wa vitabu vya Marxi kumbe vilikuwa mali ya waasi wa serikali miaka mingi kabla. Alikwenda na kusoma vitabu vile, kimoja kilikuwa na jina Karl Marx, Vladimir Lenin na Mao Zedon, lakini alichopenda zaidi kilikuwa The Times of Ezequel Zamora, kiliandikwa karne ya 19 na generali wa federal ambae Chavez alimpenda sana tangia akiwa mdogo. Vitabu hivi vilizidi kuongeza ushawishi na alinukuliwa akisema "tangia nina miaka 21 au 22 nilishajiweka kuwa mimi ni mwanaume wa mwengo wa kushoto".
Mwaka 1977, kikosi cha Chavez kilihamishiwa Anzoategui, ambako walipelekwa kupigana na kikundi cha Red Flag Prarty, kilikuwa kikundi cha Marxist-Hoxhaistin. Baada ya kuingilia kupigwa kwa waliodhaniwa askari wa kikundi hicho, Chavez alianza kuwa na mashaka jinsi jeshi lilivyotumia mbinu za kutesa. Wakati huo huo alizidi kujiingiza katika harakati za kupinga rushwa uraiani na serikalini, akiamini kwamba Wavenezuela wa kawaida hawanufaiki kutokana na mauzo ya mafuta katika nchi yao, alianza kuelewa dhana ya Red Flag Party na sababu ya mashambulizi yao.
Mwaka 1977, aliunda kikundi cha harakati za kimapinduzi pamoja na Luis R. Gonzalez an William Jimenez, akiwa jeshini, nia yake ni kuwa siku moja ataitambulisha serikali yake mpya kwa wananchi wa Venezuela; the Venezuelan People's Liberation Army (Ejercito de Liberationdel Pueblp de Venezuela au ELPV), chama hiki kilimjumisha yeye na askari wengine wachache ambao hawakuwa na mipango yeyote ya mashambulizi ya haraka pamoja na kuwa walifahamu kuwa walitaka nafasi ya kati kutoka mwengo wa kulia wa serikali na wa kushoto wa Red Flag. Pamoja na hayo alikuwa na matumaini ya kupata ushirikiano kutoka kwa wananchi waliopenda mwengo wa kushoto nchini Venezuela, Chavez aliunda mikutano ya siri ikiwa na wanasiasa wengine waliounga mkono sera za Marxi, ikiwa ni pamoja na Alfredo Maneiro (mwanzilishi wa Radical Cause) na Douglas Bravo. Wakati huu huu Chavez alimuoa msichana aliyetoka katika familia ya kawaida sana aliitwa Nancy Colmenares, ambae alibahatika kupata nae watoto watatu Rosa Virginia (aliyezaliwa September 1978), Maria Gabriela (alizaliwa March 1980) na Hugo Rafael (alizaliwa October 1983).
Maisha ya baadae jeshini na Bolivarian Revolutionary Army200; 1982-1991 Miaka miatano baada ya kuanzishwa kwa ELPV, Chavez alikwenda mbele zaidi na kuunda kikosi cha siri ndani ya jeshi, alikiita Bolivarian Revolutionary Army-200 (EBR-200), baadae alikibadilisha kuwa the Revolutinary Bolivarian Movement-200 (MBR-200). Alipendezewa na Ezequel Zamora (1817-1860), Simon Boliva (1783-1830) na Simon Rodriguez (1769-1854), ambao walijulikana kama "mizizi mitatu ya mti" wa MBR-200. Baadae, Chavez alisema kuwa "harakati za Bolivarin haikuzaliwa ije iombe ajenda za siasa...Malengo yake yalikuwa ndani zaidi. Madhumuni yake ilikuwa kwenda kwanza kujifunza historia ya jeshi la Venezuela kama chanzo cha kama chanzo cha mfumo wetu wenyewe, ambao kwa sasa haupo". Pamoja na hayo sikuzote alikuwa na matumaini Bolivarian Movement itakuja kuwa chama kikubwa cha siasa ambacho kitakubali mawazo yote kutoka mwengo wa kulia na mwengo wa kushoto na kuharibu mfumo wa kibeberu na kijamaa uliopitwa na wakati. Kwa kweli, mchambuzi mwa maswala ya kisiasa mwenye asili ya Ireland Barry Cannon aliwahi kunukuliwa akisema mfumo wa mwanzo wa MBR "ulikuwa mfumo wa kujenga kusawazisha tofauti za matabaka na kuunda tabaka moja ambalo ni la kibepari , kijamaa lakini lililokataa mawazo ya soko huria ambalo kwa wakati ule ndio lilikuwa likienezwa Latin America na pia halilikubali muundo wa Soviet Bloc ya zamani.
Mwaka 1981, Chavez akiwa kaptani, alipewa jukumu la kufundisha katika chuo cha jeshi ambapo alikuwa mwanachuo zamani. Pale aliweza kuwachukua wanafunzi wapya katika kile alichokiita mawazo ya "Bolivarian" na aliwaandikisha baadhi yao humo. Wakati wanamaliza mafunzo katika kila wanafunzi 130 angalau alipata 30 kwaajili ya mipango yake. Mwaka 1984 alikutana na Herma Marksman, mwalimu wa historia ambae ndiyo kwanza ametoka kuachana na mke wake kwa kuwa na kimada kwa muda mrefu. Katika kipindi hicho Francisco Arias Cardenas, mwanajeshi aliekuwa na shauku kwenye liberation theology (hiki kilikuwa kikundi cha dini chenye msimamo mkali kulienea Amerika ya Kusini), alijiunga na MBR-200. Cardenas alipanda cheo na kufikia cheo cha muhimu katika chama, ingawa alipingana na Chavez katika mawazo, akiamini kuwa wanaweza kuanza mashambulizi moja kwa moja kwa kupindua serikali kitu ambacho Cardenas alipinga.
Baada ya muda, baadhi ya maofisa wa jeshi walianza kustukia mbinu za Chavez na walimhamisha ili asiwe na nafasi ya kupata wanachama wapya kupitia jeshi. Alipelekwa kwenye kambi ya mbali hukuo Elorza Mkoa wa Apure, ambako alianzisha mikusanyiko na watu na kukutana na viongozi wa kikabila wa Cuiva na Yaruro. Hawakuwa na imani mwanzoni kutokana na uonevu walioupata kutoka kwa wanajeshi kabla ya hapo, Chavez aliweza kurudisha imani yao na aliungana na msafara wa vikundi vya kuboresha jamii kwenda kukutana nao. Chavez alisema baadae baada ya kukutana nao na kuelewa maisha yao ilimuwezesha kutunga sheria ya kulinda watu wale alipokuwa na madaraka. I988, baada ya kupandishwa cheo kuwa meja, Generali Rodriguez Ochoa ambae alikuwa na cheo cha juu, alimpenda Chavez na aliamuru awe msaidizi wake katika ofisi za Caracas.
Mwaka 1989 mtu aliyekuwa na siasa za kileo Carlos Andres Perez (1922-2010) alichaguliwa kuwa Rais, pamoja na kuwa aliahidi kupinga serikali ya Marekani Makubaliano ya Washington na mfumo wa International Monetary Fund's (IMF), alibadilisha kila kitu alipoingia madarakani, kilichofuatia ilikuwa soko huria na uchumi uliosaidiwa na Marekani pamoja na IMF, iliwatia hasira sana wananchi. Katika harakati za kuzuia fujo za wananchi waliopinga matumizi ya serikali, Perez alihimiza Plan Avila kama hatua za kukabiliana na fujo hizo zilizojulikana kama El Caracazo. Pamoja na kuwa wanachama wa MBR-200 walishiriki katika kuzuia fujo, Chavez hakuwepo, alikuwa mgonjwa na alilazwa hospitali akiugua chicken pox.