Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa Frank George Mwakajoka, amesema wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wamekiuka kanuni za uchaguzi kwa kuwaondoa wagombea wa chama hicho bila sababu za msingi.
Mwakajoka amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CHADEMA jimbo la Tunduma mkoani Songwe ambapo amedai hujuma zimefanyika katika maeneo mbalimbali ikiwemo mkoani Rukwa, Makambako mkoani Njombe na Tunduma mkoani.
Amesema katika maeneo hayo wasimamizi wasaidizi wametumia sababu wanazozijua wenyewe kuwaengua wagombea wa CHADEMA huku wakiwaacha wagombea wa chama tawala (CCM) ambao baadhi wameelezwa kuwa hawajui kusoma na kuandika na wengine sio wakazi wa maeneo husika waliogombea.
Soma, Pia: CHADEMA Singida: Wasimamizi Wasaidizi wa uchaguzi ndio wamewawekea wagombea wa CHADEMA mapingamizi
Hata hivyo kiongozi huyo (Makamu mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Nyasa) Frank Mwakajoka, amesema wameshakata rufaa na wanasubiri majibu na kumtaka msimamizi wa uchaguzi jimbo la Tunduma mkoani Songwe kushughulikia rufaa zao mapema iwezekanavyo ili uchaguzi ukafanyike kwa amani na utulivu na wananchi kuchagua viongozi wanaowataka.
Stella Simkonda ni mgombea ujumbe wa Serikali ya mtaa wa Msongwa Tunduma, ameeleza kushangazwa na kitendo cha kuwekewa mapingamizi ya kuwania nafasi hiyo bila sababu za msingi na bila kuelezwa waliotoa mapingamizi jambo ambalo CHADEMA wanalitaja kana kwamba ni hujuma dhidi ya wagombea wa upinzani hususani CHADEMA.
Soma: Yanayojiri kuelekea uchaguzi Serikali za Mitaa mkoa wa Mbeya