Hujuma zilikuwepo na iko siku zitasikika tu ,hilo halina mjadala ,tatizo hapa TZ bado hawa viongozi wanaoondoka na kumaliza muda wao huwa hawana la kufanya kwa ufupi huwa hawana tena kazi ,na wengi wao hawajui wafanye nini ,si watu wa biashara au wenye kumiliki viwanda ,yaani wanakuwa hawawezi kujiajiri na wanabaki katika uongozi wa nchi wakati wao si wahusika tena ,kwa ufupi huwa wanaingilia uongozi uliokuwepo na kufikia hata kuuteka nguvu au kuweza hata kuanzisha makundi.
Angalia alipoondoka Mwinyi,alipoondoka Mkapa viongozi hawa wamekuwa wakijishirikisha katika shughuli mbalimbali za serikali kikamilifu na kufikia hata kutoa hoja ,ni juzi tu katika ugombea Uraisi walijitwika na hata kuambiwa kuwa mwanzo walisusa kumkampenia Kikwete na baadae wakaibuka na kuanza kufanya kampeni katika baadhi ya sehemu.
Watu wa aina hii ni hatari sana katika nchi maana hawajiamini kuwa uongozi wao umemalizika ,sasa fikiria kama kila baada ya miaka mitano tungekuwa tunapata Raisi mpya hivi tungekuwa na msururu wa watu wangapi ?Tokea Mwiny ingelikuwa tayari wametimia watano (Tunawaita Maraisi wastaafu) Kuna Mawaziri wastaafu ,mambo ambayo watu hawa huwa hawaonekaniki katika nchi zingine ,haswa huko Maulaya ambako tunasema ndio kuna maendeleo ,hapa kwetu iweje watu hawa wawe wameganda kwenye serikali tena wakiwa na nguvu ya msukumo wa kuamrisha au kutaka kusikilizwa.
Hatujamsikia Ronald reagan wala Clinton wala Joji Kichaka na mtoto wake kujihusisha katika siasa za Marekani kwenye level za Kichama zinazoingiliana na Serikali wala ndani ya Chama au vyama vyao huwasikii kutajwa kabisa ,wanasema wakati wao umepita ,wakae wakila mafao na sikujihusisha na mambo ya serikali wala Chama.
Lakini hapa Tz hawa jamaa wanakuwa kama luba hawachezi mbali na Chama wala na serikali kote wapo ,haijulikani kama ni washauri au ni mashawishi ,ndio maana ikawa nchi yetu haiendi mbele ,maana kila mtu anapotaka kufanya ni lazima hawa jamaa wawe wenye kutia miguu ,kwenye vikao wamo,kwenye tume wamo ,hivi tutawakusanya watu wa aina hii mpaka lini ,maana mwisho wake wanaweza kutosha kuunda baraza la mawaziri.
Alichokifanya Seif Sharif ni kitu kikubwa sana na ndio hawa jamaa ndoto zao za kuivuruga Zanzibar na kubakia wao waendelee kuwa washauri wa kuchumia matumbo yao zilipopigwa na chini.
Kilichojiri Zanzibar nionavyo ni kuwa kama mliwahi kusikia kuna makundi yakipinga kuwepo kwa serikali ya umoja wa Kitaifa ,makundi au kundi hili halikuwepo Zanzibar tu hata huku Tanganyika lilikuwepo na likiwa bila ya shaka na nguvu fulani ndani ya vyombo vya dola au serikali.Sasa nia haswa na madhumuni kwa habari za hapa na pale,ilikuwa Maalim Seif akatae matokeo yaliyochakachuliwa ,wakiwa na tamaa kuwa Maalim atakataa na wananchi wataingia mabarabarani kupinga matokeo ,hapo kitatokea kitakachotokea na kutakuwa hakuna tena yale maridhiano ,yaani hata kama pasingetokea fujo ,lakini kama CUF wangeyapinga matokeo inamaama wasingekubali kuingia kwenye serikali ya umoja na wala wasingeweza kutoa makamo ,natumai hio hali mmeiona hapo au sio ?
Na kwa mtazamo wao huo wangefanikiwa kubakia katika serikali wao peke yao ,na wangekuwa na hoja kuwa CUF hivi na vile ,lakini Maalim na wenziwe walikuwa wameshaona au wameshayaona hayo kwa kitambo ,yaani walikwisha weka possibilities zote na majawabu yake na kama kawaida ilipotokea hali iliyotokea waliweza kutoa jawabu na leo hii wamo kwenye serikali na wanashiriki kikamilifu ,lile kundi limenyweaa vibaya sana .bado lipo na linajipanga lakini watu wapo macho na wanakwenda nao.