Mtoto halali na hela
JF-Expert Member
- Aug 10, 2012
- 52,160
- 48,974
Wakamatwe wote hao nyau
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukiweza nenda na health balance, itakupa clueIwe official penye kuuzwa gesi waweke mzani mamlaka mpo?
kupima sio kazi yetu, mbona wauza ngano waaminifu, wauza sabuni pia waaminifu! Kwanini wa gesi.,, waweke seal tu.Kupima sio kazi yetu, waweke seal kama za malori ya mafuta
Wakala wa vipimo mmepata activity,ple wenu mseme taasisi yenu ngumu sasa!!Iwe official penye kuuzwa gesi waweke mzani mamlaka mpo?
gas tunapigwa kinomaHujuma nzito kwa wateja, hivi ndivyo unavyoweza kusema baada ya kubainika baadhi ya wafanyabiashara wa gesi ya majumbani hupunguza kati ya kilo tatu hadi tano katika kila mtungi wanaouza.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini hujuma hiyo hufanyika zaidi mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Singida, Dodoma, Manyara, Arusha na Tanga huku Kilimanjaro ukitajwa kuwa kinara.
Kuthibitisha ukubwa wa tatizo hilo, taarifa zinaeleza kwa muda wa wiki mbili sasa, mitungi 400 ya kampuni moja ya gesi ilikamatwa mkoani Kilimanjaro ikiwa na ujazo pungufu.
Miji ya Moshi, Bomang’ombe na Himo mkoani Kilimanjaro inatajwa kuwa kinara na mamlaka zinazohusika zimeanza kulimulika suala hilo.
Mbinu wanazotumika ni wafanyakazi wa magari yanayosafirisha gesi kwenda kwenye depoti za makampuni, ambapo huipunguza njiani na kuijaza kwenye mitungi kwa siri katika baadhi ya nyumba.
Hii inadaiwa kuzisababishia hasara kampuni husika ambazo hulazimika kufidia gesi iliyopungua pale wateja wanaposhtukia huku Serikali nayo ikipoteza mapato yanayotokana na kodi.
Mbinu nyingine ni wajazaji haramu kununua mtungi mkubwa wa kilo 38 na kuijaza kwenye mitungi ya kilo 15 ambapo hupata faida ya zaidi ya Sh30,000.
Uchunguzi umebaini ujazaji huo haramu unasababisha mitungi isiwe na gesi ya kutosha kusukuma gesi yote itumike na mwisho wa siku gesi huisha wakati kukiwa na kati ya kilo mbili hadi tatu hivyo ujazaji upya huwa pungufu pia.
“Huu ujazaji ni hatarishi kwa sababu unafanyika kienyeji mitaani ambako kukitokea mlipuko madhara yake ni majanga. Kwanza wateja wanapunjwa na kuibiwa lakini ni hatari sana,” kilidokeza chanzo chetu.
Taifa Gesi, mawakala wanena
Meneja mauzo wa kampuni ya Taifa Gesi mikoa ya Kaskazini, Victor Kihwilo alikiri kuwapo kwa hujuma kwenye mitungi na Kilimanjaro ni zaidi.
“Ni kweli wiki hii tumekuwa kwenye hizo operesheni mkoani Kilimanjaro ambao ndio unaongoza kati ya mikoa yote Tanzania,” alisema.
Kutokana na hujuma hiyo, alisema kama walitarajia kuuza tani 200 mjini Moshi kwa mfano, matokeo yake huuza tani 100 mpaka 120.
Mmoja wa mawakala wa gesi, Thadey Massawe alisema kudhibiti hujuma hizo wananchi wasikubali kuchukua mtungi kabla hawajapimiwa uzito.
Ewura wafungua kucha
Meneja mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Titus Kaguo alisema uuzaji wa gesi ya kiholela ni hatari hivyo wanaimarisha ukaguzi wa kushtukiza.
“Tunafanya hivi ili kuhakikisha sheria inazingatiwa. Tunawakumbusha wananchi kufanya biashara yeyote ya petroli ikiwamo gesi bila leseni ni kosa na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika ikiwemo faini au kifungo,” alisema.
Chanzo: Mwananchi
Sheria inawataka wawe nazo, pia mnunuzi ulishauriwa usinunue gesi bila kupimwa uzito.Mbona wauzaji wengi wa rejareja hawana mizani???!
Na mizani zinachezewa pia hivyo kusoma vipimo visivyo halisi. Majizi yana mbinu nyingi. Serikali mpo ???Iwe official penye kuuzwa gesi waweke mzani mamlaka mpo?
Hizo seal zinachezewa Kaka. Wako na seal Tena ogKupima sio kazi yetu, waweke seal kama za malori ya mafuta
Na utaliwa hadi basi... Mzani ndio suluhu badala ya pombeKupima sio kazi yetu, waweke seal kama za malori ya mafuta
Kwanini za matanker ya mafuta na meter za Tanesco hazichezewi?Hizo seal zinachezewa Kaka. Wako na seal Tena og
Kwani huo mzani ndio hauna seal ya wakala wa vipimo?
Sasa seal ya Tanesco hata ukiichezea utaokoa sh ngapi?Kwanini za matanker ya mafuta na meter za Tanesco hazichezewi?
Kwani kwenye mitungi unaibiwa shs.ngapi, milioni au? Na kwenye mitungi kwani hawana kiwango max. cha kuiba? Anaweza akaiba hadi mteja akibeba ashtuke?Sasa seal ya Tanesco hata ukiichezea utaokoa sh ngapi?
Matanker pamoja na kwamba Kuna seal lkn hata wavunje seal haisaidii kwani Kuna maximum allowable loss due to temperature. Yakipungua zaidi ya allowable loss hata Kama seal iko intact pingu zinamhusu dereva
Kwa mimi binafsi mtaa mnao ishi vijiwe vya kuuzia gess vipo vingi sana ila sijawahi kuona kituo chenye mizani kwa huku kitaa