Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,281
Anaandika Mdau kutoka Mwanza
HUJUMA ZA KUTISHA UCHAGUZI MKUU WA BAWACHA - MWANZA
Leo 18 May 2021 ni siku ya Uchaguzi Mkuu wa Bawacha Taifa kujaza nafasi zilizoachwa wazi na akina Halima Mdee na wenzie, Kwa tulio wengi tunategemea Chadema kama Chama cha Demokrasia na waumini wakubwa wa uhuru katika Chaguzi wangesimamia Haki ya Uhuru katika Uchaguzi huo kinyume kabisa na matarajio, Uchaguzi huo umegubikwa na hujuma nyingi sana.
Taarifa za Uhakika ni kwamba Sekretarieti ya Chama ina mgombea wake inayetaka ashinde hata kwa goli la mkono na tayari Timu nzima ya Secretariet ya Chama iko Mwanza kuhakikisha Mtu wao anashinda.
Jambo la kushangaza ni kwamba hata baadhi ya wajumbe wa kamati kuu wakiongozwa na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa na Mbunge toka Kanda ya Serengeti wako Mwanza na wanafanya Kampeni dhidi ya Mgombea wao wanayemtaka huku wakichafua wagombea wengine.
Taarifa za Uhakika zinasema ndani ya Uchaguzi huu kuna vita kubwa sana kati ya Kundi la waliokuwa wabunge wa Viti maalumu Chadema 2015 ambao wanamuunga Mkono Catherine Ruge ambaye alikuwa Mbunge mwenzao Vs Ester Daffi ambaye anatizamwa na Kundi la wanawake wa kawaida kama mtu ambaye ana uwezo wa kuunganisha wanawake na kuvunja Makundi.
Wanawake wengi ndani ya Chadema wanaamini kufukuzwa kwa Halima Mdee na wenzake ni Fursa ya kujenga upya baraza hilo ambalo lilikuwa na makundi makubwa mawili (Kundi la wanufaika wa Fursa za Baraza Vs Kundi lisilostahili kunufaika)
Wanawake wengi wa kawaida wanaamini Waliokuwa wabunge ni wanufaika wakubwa wa Fursa za Baraza hilo na ndio mana wanamuunga mkono aliyekuwa Mbunge mwenzao Catherine Ruge kuwa Katibu Mkuu ili waendelee kulinda Fursa zao za kuendelea kuwa wabunge.
Katika Uchaguzi huo unaofanyika leo Wajumbe wa secretariet wamepanga Yafuatayo.
1. Kura zisihesabiwe ukumbini kinyume na utaratibu wa siku zote ili wapate Fursa ya kuiba kura.
2. Wamepanga kuingiza wajumbe Fake kwenye kikao cha Uchaguzi.
3. Wamepanga Timu ya kugawa Fedha kwa wapiga kura ili Catherine Ruge ashinde na Timu hiyo inaongozwa na Suzan Limo aliyekuwa Mbunge wa Viti maalumu Chadema toka 2005 Mpaka 2020 Pamoja na Suzan Kiwanga aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mlimba , zoezi hilo linafanyika Vizano Hotel hapa Mwanza na wajumbe wanaitwa na kupewa Fedha .
4. Wamepanga kuwatoa nje ya ukumbi wa Uchaguzi wapiga kura ambao hawawaungi Mkono.
WITO Wangu.
1. Tunamuomba Mh John Mnyika kuingilia kati jambo hilo mana hujuma za kuharibu Uchaguzi zinafanywa na wasaidizi wake na yeye ndio Mgeni rasmi kwenye Uchaguzi huu , itakuwa aibu kubwa kwake anayehubiri uhitaji wa Tume huru ya Uchaguzi kila siku kushindwa kusimamia Uchaguzi huu kwa uhuru.
2. Wajumbe kamati kuu ya Chadema wakae mbali na Uchaguzi huu wameshachuja majina wamemaliza kazi zao hawawezi kuchuja majina ya wagombea alafu wanaenda Mwanza kufanya Kampeni ni kinyume na Katiba na ushahidi upo kutosha zikiwepo picha na video tena miongoni mwao ni wanaume lakini wanafanya Kampeni za wanawake na wako huko Mwanza.
3. HUJUMA za Rushwa zinachafua Chama hivyo Mnyika kama Katibu Mkuu ashugulikie kikatiba hawa wote wanaotoa Rushwa ambao bila shaka anawajua mana ni wasaidizi wake na wengine ni wajumbe wa kamati kuu.
NB: UCHAGUZI HUU LEO UKIHARIBIKA CHADEMA ITAKOSA UHALALI WA KUDAI TUME HURU YA UCHAGUZI NA SISI WANAWAKE HATUTAKUBALI KABISA KUHUJUMIWA.