Maswa Yetu
Senior Member
- Mar 18, 2023
- 155
- 217
Mpaka sasa nchi nzima tunakubaliana kwamba utendaji wa serikali unazorota kila kukicha, wafanyakazi wa serikali wanafanyakazi wanavyojisikia, kama hauamini hili subiri utakapopata shida ya kukutana na watendaji wa serikali ndiyo utaelewa.
Kwa tathimini ya haraka kiongozi anayejielewa, anayeheshimika na wananchi wa rika zote, dini zote, vyama vyote ni waziri mkuu Kassim Majaliwa .Hata wapinzani kama Chadema huwa hawamsemi vibaya Kassim Majaliwa.
Kwenye serikali nzima ya Rais Samia ni Kassim Majaliwa tu ndiyo anapofanya ziara sehemu viongozi huwa wanaogopa madudu yao kuibuliwa, hata wananchi wa kawaida kabisa (wanyonge) wakimuona Kassim Majaliwa hupata faraja kwamba angalau shida zao zitasikilizwa.
Viongozi wengine hata wanapofanya ziara hamna anayewaogopa maana hawatatui wala kusikiliza kero yoyote ya wananchi zaidi ya kupongezana na kugawana posho tu.
Naamini kama watanzania watamfanya Kassim Majaliwa kuwa rais wao ,utendaji wa serikali utabadilika sana na watu wataanza kuchapa kazi kama enzi ya Rais Magufuli.