o_2
JF-Expert Member
- Jul 20, 2017
- 428
- 385
Habari za mausiku,
Mmelala sio, mkiamka mtaikuta.
Jana nilianza safari kutokea Tukuyu kwenda Tanga. Tukuyu, Busokelo ndani ndani huko. Ipo changamoto ya usafiri ya hatari. Na kama unavyojua shule zinafunguliwa kwa hiyo usafiri ni 'mtihani' kwelikweli. Bahati mbaya zaidi hakuna basi la moja kwa moja kutokea Tukuyu-Tanga halipo.
Basi bwana nikaanza safari yangu mdogo mdogo kwa kupanda 'Noah' kutokea Busokelo mpaka Tukuyu, baada ya hapo nikapanda 'coaster' mpaka Mbeya city, stendi kuu.
Nikawaza leo nataka nile winga mpaka 'morning' . Silali lodge. Muda unavyokwenda baridi inaongezeka, basi nikafikiria kununua chai ya moto, kahawa basi ilimradi tu ujoto ujoto uje mwilini.
Basi wapo wamama wamejipanga, unachagua tu, mmama wa kwanza nikamsalim, nikapita kwa mmama mwingine kupata nilichokuwa nakihitaji. Nikakikapata. Lakini mmama wa kwanza alikua na jiko la mkaa linawaka kama mwenge. Nikaona isiwe tabu zaidi, nikamuomba, "Samahani, naweza kukakaa kwenye benchi lako niotee moto kidogo?" Mmama kaniangalia tu kauzu kweli kweli. Nikamuomba tena akakubali.
Nikakaa, nikainjoy joto la 'abuja' raha sana kutokana na baridi iliyokuwepo. Nikamaliza pale, nikaendelea kuzunguka zunguka kidogo kushangaa mazingira. Baadae nikaona mwili umepata ubaridi. Nikarudi tena kwa mmama yule, nikamuomba tena...
Mmama amenikatalia katu katu, usikae hapa kaa kule, wewe si ulikuwa umekaa kule.
Ye!!!??
Nikaona isiwe bugudha, yule mmama mwingine kusikia yule mmama ananiambia vile akaniambia njoo ukae hapa. Basi bwana nikaenda kukaa na nikanywa chai na alikuwa na moto.
Saa hizi ni saa 2:07 usiku, bado na vutavuta muda ifike saa 05:30 asubuhi safari ikaanze.
Roho nyeusi zipo na Roho nyeupe zipo.
Tuishi.