Huko kwenye chama chenu nani sio msaliti? Nani ni muaminifu?

Huko kwenye chama chenu nani sio msaliti? Nani ni muaminifu?

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2013
Posts
8,586
Reaction score
11,227
Nauliza Kwa Nia nzuri tuu Inamaana chama chenu ni ngome ya wasaliti? Nauliza huku kwetu msaliti nani mbona simkumbuki hata mmoja? Je nani kwenu ni muaminifu katika mliopo?

Alikuwapo shujaa Chacha wangwe kamanda kweli kweli! Mwamba asiyeogopa kitu. Bila shaka mnamkumbuka lakini huyu nae mkaja kutuambia ni msaliti akaingia kwenye mgogolo mzito sana na kipenzi chetu mwenyekiti Mbowe. Sakata hili lilimalizika Kwa ajali ya utata ya kamanda huyu msaliti!! Huzuni

images (21).jpeg


Alikuwepo Zitto kabwe wa CHADEMA. Kamanda huyu kichwa kimoja kilikuwa sawa sawa na wabunge wote wa CCM pale Dodoma. Alikuwa na uwezo wa kuondoka na Kijiji! Kwa wakongwe wa siasa wanakumbuka moto wa mwamba huyu aliyewahi kukwepa kwepa kwenye ajali njombe ikamtoa Salome Mbatia.Mwamba kweli kweli.

Huyu nae alipo kitishia kile kiti Cha enzi eti mmetuambia ni msaliti anatumiwa na CCM?? Nani sio msaliti huko Kwa chama chenu??
images (22).jpeg


Aliondokea Dr Kitila Mkumbo Kwa wakati ule . Mbabe wa siasa za ubungo asiye mbabaifu.. nani anamkumbuka mtabe huyu wa siasa za kisomi?

Nasikia mlimsema kuwa nae ni CCM naona akaitikia yupo huko anaitumikia serikali.

DSC00331.JPG


Kaondokea mwamba wa Karatu, Dr wilbload Slaa na mchumba wake mushumbusi mnamkumbuka hii! Huyu mwamba ukisikia CHADEMA kwenye vitongoji ujue ndio kazi yake mwaka 2010.. mwamba kweli kweli asiye mbabaifu. Alitimka CHADEMA baada ya Ayatollah kung'ang'ana kumpokea fisadi kugombea uraisi Kwa tiketi ya chama chenu miaka Ile...

Huyu nae hakuna kazi yake njema inayokumbukwa pale CDM inasemekana tuu kuwa ni msaliti na amekuwa akikihujumu chama Kwa muda wote.
images (23).jpeg

Huko kwenu nani sio msaliti nani ni muaminifu??

Niliwahi kufikiria kuwa ni mchungaji Peter Msigwa. Kamanda kweli kweli... Mlaumbwa huyu amekitikisa sana chama Cha Mapinduzi kwenye siasa za Iringa hata za ndani ya CCM! Mwamba kweli kweli.. nasikia nae ni msaliti na ameunga juhudi??

Nani ni muaminifu huko kwenu?
images (25).jpeg


Kwenye siasa za mapambano utamkwepaje Halima mdee mwamba wa Dar es salaam.. mpambanaji huyu ameshuhudia mpaka vipigo kwenye mambo ya mapambano alikuwa mwanaume kweli kweli! Nasikia yeye pamoja na Genge la vigogo wa CHADEMA 17 wote woteee ni wasaliti Tena ni CCM! Huko kwenu nani ni muaminifu

images (26).jpeg


Huko kwenu alikuwepo Joshua Nassari.. mwanasiasa pekee mkweli baada ya baba wa Taifa Tangu kutengenezwa Kwa Taifa letu. Aliibiwa ubunge mwaka 2010 akarudishiwa na Mungu mwaka 2012.. siasa za Arumelu Mashariki nani amesahau??

Huyu nae aliyepitishwa Kwa jasho la akina mama wa sokoni nasikia ni msaliti Tena mnafiki mkubwa na ameunga juhudi yupo CCM.. hivi kama Joshua Nassari yule... Nani ni muaminifu huko Kwa chama chenu?
images (24).jpeg


Aliondokea wakili msomi Tundu Lisu. Nakumbuka mlituaminisha kuwa mwamba huyu Akili yake labda tujumlishe Akili za Wana CCM wote nchi hii nikiwemo na mimi.
Nasikia eti Lisu nae aliyepigwa Risasi 17 ni msaliti na anatumika kumuhujumu mtukufu Ayatollah Mbowe Khomeini.
Tundu_A._M._Lissu.jpg

Wajuvi wa mambo mniambieni nini kingetokea Chadema isingetifuana miamba kweli kweli hii ingekaa meza Moja?

Nataka kujiunga Chadema Leo saa Saba mchana ila naogopa maana sijui nani asiye msaliti kwenu sielewi nani ni muaminifu huko kwenu.. nisije nikaingia huko na mimi nikawa msaliti. Naomba kujibuwa wajuvi wasiasa nyie.

Ahsante
 

Attachments

  • images (24).jpeg
    images (24).jpeg
    26.9 KB · Views: 2
Nawakumbusha tu kuna mstari unaimbwa "mpaka waisome namba eee" mpaka leo bado haijasomwa iyo namba
 
Back
Top Bottom