Huko Nyakato Mwanza tuliambiwa kuna mitambo ya kuzalisha MW 80 kwa kutumia dizeli. Kwanini sasa isiwashwe kwenye kipindi hiki cha uhaba?

Dr Akili

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Posts
5,119
Reaction score
4,569
Nadhani ni kwenye awamu ya nne ya JK, mitambo ya kuzalisha MW 80 ilisimikwa huko Nyakato Mwanza ya kutumia mafuta ya dizeli kwa gharama ya mabilioni mengi ya pesa. Mahitaji ya umeme ya jiji la Mwanza hayazidi MW 3, hivyo MW hizo 80 zinatosha kwa matumizi ya kanda yote ya Ziwa Victoria ie mikoa ya Mara, Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Kagera hadi Kigoma.

Katika kipindi hiki cha uhaba wa umeme na kusabisha mgawo mkali, kwa nini mitambo hiyo ya Nyakato isiwashwe? Katibu mkuu wa wizara ya nishati (Bw. Mramba) atakuwa anaijua vizuri mitambo hiyo kwani alikuwa part ya usimikaji wake akiwa Mkurugenzi mtendaji wa tanesco kipindi hicho. Huyu CEO wa sasa, Bw. Maharage anapaswa kuijua na kuiendeleza. Bomba la gesi kabla ya kupelekwa nchi jirani for export, linapaswa kuja kwanza Mwanza kwa matumizi ya mitambo kama hiyo na matumizi mengineyo hususani ya viwanda katika kanda hii ya maziwa makuu yenye wakazi wasiopungua asilimia 30% ya watanzania wote.

Kwa nini mitambo hii haiwashwi na wala tanesco na wizara ya nishati haiiongelei? Nini kiliipata mitambo hii iliyotugharimu matrilioni ya pesa za walipakodi? Tuliwahi kusikia kwenye awamu ya tano kwamba kupitia mikataba mibovu, gesi yetu ya kutoka Songosongo umilki wake (control) uko mikononi mwa makampuni ya nje hususani ya Symbion na yaliyojenga hilo bomba ya gesi hadi Kinyerezi.

Hata hiyo mitambo ya kuzalisha umeme kwa majenereta ya dizeli huko mkoa wa Kigoma waliyoyazima hivi karibuni kwa mbwebwe, yanapaswa kuwashwa kwenye kipindi hiki cha uhaba. Hii haihitaji utalaamu wa umeme, it is just common sense logic.
 
We uliamini?
Ni kweli hiyo mitambo ipo hapo Nyakato. Kama huamini nenda kaiangalie. Hili halina ubishi. Ipo pale idle. Sijui kama inafanyiwagwa service na kama baadhi ya vipuri vyake vilishanyofolewa. Tanesco wanapaswa kuwajuza wananchi kwani pesa yao ya kodi ilitumika pale. CAG naye anapaswa kwenda kuikagua na kuitolea ripoti kwenye bunge la wananchi ili liweze kuibana serikali kwa mjibu wa katiba ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…