Huku Diamond na wenzake, kule Reginald Mengi na wenzake!

Huku Diamond na wenzake, kule Reginald Mengi na wenzake!

reandle

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2009
Posts
11,166
Reaction score
8,148
Watu wanamwaga povu kisa Diamond na baadhi ya wasanii wamejitokeza kuipigia kampeni CCM na madai yao ni kwamba wasanii ni wasaliti wa mabadiliko!! Guys, are serious?! Hivi ni kwamba hatufahamu kwamba wasanii kazi zao za sanaa ndo biashara yao, au? Ikiwa Diamond na wenzake ni wasaliti, what about Reginald Mengi, Bakhresa na wenzake ambao wametumia vituo vyao vya TV kutangaza kampeni za CCM nchi nzima? Kama kinachotusukuma sio ulimbukeni wa kisiasa mbona hatujitokezi kuwashambulia akina Mengi wanaotumia media zao kuitangaza CCM?

Wapo watakaosema kwamba akina Diamond ni vijana, so walitakiwa kuyaunga mkono mageuzi... kama ndivyo, je kuna vijana wangapi walioachia ngazi kwenye hizo TV Stations kv tu hawakutaka kufanikisha zoezi hilo? Hivi mngekuwa nyinyi ndo wanamuziki halafu mkapewa mchongo na CCM, hivi kweli mngekataa au mnataka wenzenu ndo wakatae? Hivi leo hii CCM wakienda kukodi ukumbi wa Club Billicanas mnatarajia Mbowe atakataa?! Kuna wengine eti wanahamasisha watu kususia kazi za wasanii... kwanini wasisusie biadhaa za watu kama akina Bakheresa? Hivi kabla mtu hujajishughulisha kupiga kampeni ya kususia kazi za wasanii, umeshajiuliza mwaka huu umetumia shilingi ngapi kununua kazi zao zaidi ya kwenda kupiga yowe kwenye pages zao contrary na pesa ulizotumia mwaka huu kununua bidhaa za akina Bakheresa, Mengi, Diallo na wenzake?

Wala hapahitajiki shahada ya chuo kikuu kufahamu kwamba hakuna msanii hata mmoja (ukiondoa wale walio jukwaa la siasa moja kwa moja) ambae angeweza kupewa mchongo na CCM halafu akakataa... HAKUNA! Mtu kama Ali Kiba hakuonekana, mosi inawezekana mchongo hakuupata au inawezekana vilevile muda wake bado coz' kampeni ndo kwanza zimefunguliwa! Au inawezekana CCM hawakuona sababu ya kuwachukua mafahari wote wawili but there's no way kwamba amekataa! Na akiwa alipewa mchongo na akakataa wala sina sababu ya kumsifia zaidi ya kumuona ni mpumbavu coz' yeye muziki ndo kazi yake... unapofanya biashara huwezi kuchagua mteja!

Wanasiasa wenyewe wapo kimaslahi zaidi kwahiyo ni kiroja kuwataka wasanii ndo wawe "wazalendo" zaidi lakini wengine wote business as usual!! Hivi hatujiulizi ni kwanini hata hao UKAWA linapokuja suala la posho bungeni huwa wanaongea lugha moja na CCM? Ni nini kama sio all about maslahi ya mifuko yao? Sasa how come mtake wasanii pekee ndo wa-sacrifice!! Hivi leo hii CCM wanapojisifia kwamba tumefanya hiki au kile; hizo kazi zinafanywa na nani kama sio na sisi sisi? Hivi leo hii vijana wooooooooote wakisusa kufanya kazi serikalini, je serikali itabaki madarakani angalau kwa wiki moja kabla ya kuporomoka? Kwanini tusianze sisi wenyewe kususia kufanya kazi na serikali ya CCM?

Wapo watakaosema wasanii hawakutakiwa kuchukua upande kwavile wana mashabiki wenye itikadi mbalimbali! Kauli kama hizo ni za kinafiki coz' najua wengi wao kama sio wote tatizo sio msanii kuchukua upande bali msanii kuchukua upande ambao yeye (shabiki) hauungi mkono! Tunachotaka tunachounga sisi mkono ndicho na yeye (msanii) aunge... eh! Kama msanii fulani humpendi basi akiunga mkono chama usichokipenda ndo anakufanya umchukie zaidi... MAAJABU HAYA!

Tangu niingie JF miaka kadhaa iliyopita sijawahi kubadili msimamo wangu kwamba CCM na UPINZANI wote ni wale wale tu... wote ni WEZI tu!

ENDELEENI KUPIGA SIASA ZA KWENYE SOCIAL MEDIA WAKATI WENZENU WANAPIGA PESA... Recall Sugu Vs Ruge saga! Na kama unatarajia akiingia madarakani fulani mambo kwako yatakuwa mepesi au kutakuwa na mabadiliko then you're done unless you stop talking like politicians wakati wenzenu wapo kazini!

UPDATE:
Kwa hisani ya Mkuu Mr Hero akanikumbusha haya hapa chini:

Ndesa.jpg

Ndesapesa tena, huyu hapa
 
Last edited by a moderator:
Hahahahaaaa! JF wame-delete post kwavile nimewaambia na wao ni wasaliti wa mabadiliko!!!!
 
Duh! Nilikuwa sijaingia JF muda mrefu... kumbe hata JF napo kuna bango la kampeni za CCM?! Invisible na wenzako bila kumsahau Maxence Melo, nyie jamaa ni wasaliti wakubwa wa mabadiliko! How come mnatuwekea mabango ya CCM hapa wakati hili jamvi linatembelewa na watu wenye itikadi tofauti?

Tumeshapigwa bei ya jumla jumla ccm wanakwambia mbele kwa mbele, wewe kama unawaza maendeleo ni upumbavu na ulofa wako huo.
 
Last edited by a moderator:
umeandika pumba tupu na sijaelewa inakuwaje umekuwa kilaza kiasi hicho ITV ikirusha mkutano wowote live au recorded tofauti na kwenye taarifa ya habari au makala nyingine za kawaida ujue hiyo airtime imenunuliwa na chama husika na wala sio meneja anatangaza bure, they are paying a lot of money to buy airtime its not for free.
 
Aisee! Unapenda shari ile mbaya! Kwahiyo ewe Genius mwenye full miakili, ITV kufanya biashara sawa, lakini wasanii sio sawa? Au Mr. Genius mwenye akili kibao unadhani watu wanapiga show kama sadaka?!

JF The Home of Greatest Thinkers!!!
 
Tumeshapigwa bei ya jumla jumla ccm wanakwambia mbele kwa mbele, wewe kama unawaza maendeleo ni upumbavu na ulofa wako huo.
Lakini Matola let's be honest huku tukijua Mungu anatuona! Hivi Matola wewe unavyoipiga za uso CCM leo hii assume una mabasi kadhaa halafu wakakupa pesa ya kutosha wanataka mabasi yao wakafanyie kampeni utakataa?!
 
Umeongea point Wabongo bwana wanaleta mambo ya diamond na alikiba kwenye siasa. Hata mtu yoyote lipite basi linasema elfu 30 ukienda jagwani kwa jili ya kupiga kampeni kuna mwenye njaa humu hata kataa hebu watu acheni mambo yenu bhana wasani sanaa ndo inawalisha watakataa je. Na kwanza vyama vya siasa ni kama dini kila mtu ana haki ya kuchagua anacho taka
 
Kichinjio ninacho, tutaheshimiana tu.
 
Attachments

  • 1440390399219.jpg
    1440390399219.jpg
    40.6 KB · Views: 816
Chige nadhani sio suala la kuperform watu ndio wanatofautiana nae domo ni suala la yeye kukomaa huko kwenye social media (instagram) kuipigia kampeni CCM .Anyway ana uhuru binafsi ,,lakini narudia sio suala la kuperform Ila ni anapokuwa mpiga kampeni wa CCM ..Kama ex wake Wema na hapo atakumbana na upinzani wa washabiki wake ambao hawaungi mkono chama anachokipigia kampeni ( vile vile hata angeipigia kampeni Ukawa bado washabiki wake wa CCM wangetofautiana nae)
 
Umeongea point Wabongo bwana wanaleta mambo ya diamond na alikiba kwenye siasa. Hata mtu yoyote lipite basi linasema elfu 30 ukienda jagwani kwa jili ya kupiga kampeni kuna mwenye njaa humu hata kataa hebu watu acheni mambo yenu bhana wasani sanaa ndo inawalisha watakataa je. Na kwanza vyama vya siasa ni kama dini kila mtu ana haki ya kuchagua anacho taka
Umeona enh! Waislamu wanauza kiwanja kwa Walokole wajenge kanisa and vice versa halafu mtu awasimange wasanii kupiga show za CCM!!!!
 
Aisee! Unapenda shari ile mbaya! Kwahiyo ewe Genius mwenye full miakili, ITV kufanya biashara sawa, lakini wasanii sio sawa? Au Mr. Genius mwenye akili kibao unadhani watu wanapiga show kama sadaka?!

JF The Home of Greatest Thinkers!!!
of course yes i am a great thinker and genius as well too, domo ni public figure and is there for all fans regardless their political affiliations, to please and entertain the public as one is to not rely on any alliance.

mengi kazi yake ni kumake money kwenye media and politics is about media na sheria na maadili ya biashara yake yanamruhusu and mengi sio public figure he's just a business man anachotakiwa kufaanya ni kuwavutia wateja wake wanaompelekea hela kwa kutoa huduma bora za matangazo basi na wala hayupo close na jamii kama msanii ambaye yeye an deal na jamii direct and physically solely.

mengi ni company manager or member of the body of directors anaweza asiwe na umiliki wa kampuni ya IPP 100% bali ni kwa share fulani hivyo miradi yake haiendeshwi na yeye kama yeye kwa 100% and on top of that that is different business far from music, you got to know that.
 
Chige nadhani sio suala la kuperform watu ndio wanatofautiana nae domo ni suala la yeye kukomaa huko kwenye social media (instagram) kuipigia kampeni CCM .Anyway ana uhuru binafsi ,,lakini narudia sio suala la kuperform Ila ni anapokuwa mpiga kampeni wa CCM ..Kama ex wake Wema na hapo atakumbana na upinzani wa washabiki wake ambao hawaungi mkono chama anachokipigia kampeni ( vile vile hata angeipigia kampeni Ukawa bado washabiki wake wa CCM wangetofautiana nae)
Sawa... hapa ndipo tunajifichia but who knows? Ikiwa mkataba wake unahusisha kampeni hadi kwenye social networks tunatarajia angekataa hata kama amepewa kisu cha kutosha?
Tusisahau kwamba hata CCM wanafahamu kwamba ukitaka kuwapata vijana basi kampeni ziende hadi kwenye social networks!!Labda ushauri ingekuwa ni kutumia a/c nyingine lakini kila advertiser analipia a/c yenye followers wengi and not otherwise! But all in all, hoja inarudi pale pale... ingekuwa ndo sisi ndo wasanii wenyewe, je tungeweza kuzi-turn down hizo deal?

Kitu pekee ambacho sijakipenda ni pale alipoandika "Hivi hatujiulizi ni kwanini viongozi wote ni wa kabila lile lile...!" Hii hata mimi alinikera na pale pale nilimchana lakini inaelekea watu wamemwambia kwamba hiyo ni kauli ya kipumbavu manake sijaiona.... itakuwa amefuta!
 
of course yes i am a great thinker and genius as well too, domo ni public figure and is there for all fans regardless their political affiliations, to please and entertain the public as one is to not rely on any alliance.

mengi kazi yake ni kumake money kwenye media and politics is about media na sheria na maadili ya biashara yake yanamruhusu and mengi sio public figure he's just a business man anachotakiwa kufaanya ni kuwavutia wateja wake wanaompelekea hela kwa kutoa huduma bora za matangazo basi na wala hayupo close na jamii kama msanii ambaye yeye an deal na jamii direct and physically solely.

mengi ni company manager or member of the body of directors anaweza asiwe na umiliki wa kampuni ya IPP 100% bali ni kwa share fulani hivyo miradi yake haiendeshwi na yeye kama yeye kwa 100% and on top of that that is different business far from music, you got to know that.
Do I need to remind you Diamond isn't a gospel singer? By the way, ikiwa Mengi anaruhusiwa kisheria na kimaadili, ni sheria ipi na ya wapi inakataza msanii kuuza huduma zake za kisanii kwa chama cha siasa? Ina maana hadi leo hufahamu kwamba mwanamuziki nae n mfanyabiashara mr. genius?
 
Aisee! Unapenda shari ile mbaya! Kwahiyo ewe Genius mwenye full miakili, ITV kufanya biashara sawa, lakini wasanii sio sawa? Au Mr. Genius mwenye akili kibao unadhani watu wanapiga show kama sadaka?!

JF The Home of Greatest Thinkers!!!

Ndugu yangu madhara ya mwanamuziki kujiingiza kwenye ushabiki huwezi yaona sasa hivi lkn subiri ili vuguvugu la uchaguzi liishe ndo utaona!!

Kama mwanamuziki alitakiwa asionyeshe ushabiki wa chama chochote ili aendelee kuwakamata mashabiki wote bila kujali itikadi zao!

Alichokosea Diamond ni kuanza kupost mambo ya ushabiki wa siasa ktk account zake za facebook na instagram
 
leo siku yangu itakua poa sana nimeamka na kukuta uzi ulioenda shule nikapata na tabasam juu,wapumbavu watajazana kuponda wao wanasomaga intro tu
 
Back
Top Bottom