Huku Diamond na wenzake, kule Reginald Mengi na wenzake!

Huku Diamond na wenzake, kule Reginald Mengi na wenzake!

Watu wanamwaga povu kisa Diamond na baadhi ya wasanii wamejitokeza kuipigia kampeni CCM na madai yao ni kwamba wasanii ni wasaliti wa mabadiliko!! Guys, are serious?! Hivi ni kwamba hatufahamu kwamba wasanii kazi zao za sanaa ndo biashara yao, au? Ikiwa Diamond na wenzake ni wasaliti, what about Reginald Mengi, Bakhresa na wenzake ambao wametumia vituo vyao vya TV kutangaza kampeni za CCM nchi nzima? Kama kinachotusukuma sio ulimbukeni wa kisiasa mbona hatujitokezi kuwashambulia akina Mengi wanaotumia media zao kuitangaza CCM?

Wapo watakaosema kwamba akina Diamond ni vijana, so walitakiwa kuyaunga mkono mageuzi... kama ndivyo, je kuna vijana wangapi walioachia ngazi kwenye hizo TV Stations kv tu hawakutaka kufanikisha zoezi hilo? Hivi mngekuwa nyinyi ndo wanamuziki halafu mkapewa mchongo na CCM, hivi kweli mngekataa au mnataka wenzenu ndo wakatae? Hivi leo hii CCM wakienda kukodi ukumbi wa Club Billicanas mnatarajia Mbowe atakataa?! Kuna wengine eti wanahamasisha watu kususia kazi za wasanii... kwanini wasisusie biadhaa za watu kama akina Bakheresa? Hivi kabla mtu hujajishughulisha kupiga kampeni ya kususia kazi za wasanii, umeshajiuliza mwaka huu umetumia shilingi ngapi kununua kazi zao zaidi ya kwenda kupiga yowe kwenye pages zao contrary na pesa ulizotumia mwaka huu kununua bidhaa za akina Bakheresa, Mengi, Diallo na wenzake?

Wala hapahitajiki shahada ya chuo kikuu kufahamu kwamba hakuna msanii hata mmoja (ukiondoa wale walio jukwaa la siasa moja kwa moja) ambae angeweza kupewa mchongo na CCM halafu akakataa... HAKUNA! Mtu kama Ali Kiba hakuonekana, mosi inawezekana mchongo hakuupata au inawezekana vilevile muda wake bado coz' kampeni ndo kwanza zimefunguliwa! Au inawezekana CCM hawakuona sababu ya kuwachukua mafahari wote wawili but there's no way kwamba amekataa! Na akiwa alipewa mchongo na akakataa wala sina sababu ya kumsifia zaidi ya kumuona ni mpumbavu coz' yeye muziki ndo kazi yake... unapofanya biashara huwezi kuchagua mteja!

Wanasiasa wenyewe wapo kimaslahi zaidi kwahiyo ni kiroja kuwataka wasanii ndo wawe “wazalendo” zaidi lakini wengine wote business as usual!! Hivi hatujiulizi ni kwanini hata hao UKAWA linapokuja suala la posho bungeni huwa wanaongea lugha moja na CCM? Ni nini kama sio all about maslahi ya mifuko yao? Sasa how come mtake wasanii pekee ndo wa-sacrifice!! Hivi leo hii CCM wanapojisifia kwamba tumefanya hiki au kile; hizo kazi zinafanywa na nani kama sio na sisi sisi? Hivi leo hii vijana wooooooooote wakisusa kufanya kazi serikalini, je serikali itabaki madarakani angalau kwa wiki moja kabla ya kuporomoka? Kwanini tusianze sisi wenyewe kususia kufanya kazi na serikali ya CCM?

Wapo watakaosema wasanii hawakutakiwa kuchukua upande kwavile wana mashabiki wenye itikadi mbalimbali! Kauli kama hizo ni za kinafiki coz' najua wengi wao kama sio wote tatizo sio msanii kuchukua upande bali msanii kuchukua upande ambao yeye (shabiki) hauungi mkono! Tunachotaka tunachounga sisi mkono ndicho na yeye (msanii) aunge... eh! Kama msanii fulani humpendi basi akiunga mkono chama usichokipenda ndo anakufanya umchukie zaidi... MAAJABU HAYA!

Tangu niingie JF miaka kadhaa iliyopita sijawahi kubadili msimamo wangu kwamba CCM na UPINZANI wote ni wale wale tu... wote ni WEZI tu!

ENDELEENI KUPIGA SIASA ZA KWENYE SOCIAL MEDIA WAKATI WENZENU WANAPIGA PESA... Recall Sugu Vs Ruge saga! Na kama unatarajia akiingia madarakani fulani mambo kwako yatakuwa mepesi au kutakuwa na mabadiliko then you’re done unless you stop talking like politicians wakati wenzenu wapo kazini!

UPDATE:
Kwa hisani ya Mkuu Mr Hero akanikumbusha haya hapa chini:

View attachment 279756

Ndesapesa tena, huyu hapa

You're very right boss...I have nothing more/ less.
 
Last edited by a moderator:
Kama niliwahi kubisha diamond ni msanii mkubwa sana naomba mnisamehe. ..
Ah, we Muuza Sura long time nafahamu unamkubali Chibu sema tu kuna kipindi sijui ulikuwa unampigia misele demu wa Team Kiba hapa JF na wewe ukajifanya Team Kiba kama ambavyo Matola alipoanza kujifanya Team Kiba kumbe alikuwa anapigia minyato dea la t-shirt.. just kidding!
 
Wanaomlaumu Diamond bado hawajui lack of education. Kama amethubuti kuongea mbele ys Rais kwamba yeye kuzaa na Zari ni maendeleo kwa Taifa hakuna atakalolifanya anishangaze.
 
hahahahha!mimi Team Kiba bab mwanzo mwisho!wanachokosea watu wengi ni msanii mwenye jina kubwa na msanii mwenye kipaji kikubwa!chibu ana jina kubwa ila kiba ana kipaji kikubwa!lakini yote ya yote tukiachana na mziki namkubali sana chibu anavyowakomesha vijana wanaotaka kuvimbiana naye mtaani!....vita ya mtaani si ya chibu na kiba!ni chibu na team mahips mporomoko wema sepetu na takataka zingine za mademu tasteless na watoto wa kiume wanaoishi kwa migongo ya wanawake na upambe wakati chibu anahustle kinigga
 
True kwa 99%... nimetoa 1% kwa sababu ulitakiwa kumalizia kabisa mwenye kipaji kikubwa ambae alibweteka na kipaji chake hadi alipokuja kukurupushwa usingizini! Leo hii Diamond anakuwa ndo wa kuonesha njia wakati alitakiwa kufuata njia ya wakongwe na talented kama Ali. Majority ya mashabiki wa Diamond walikuwa ni wa Ali Kiba. Anyway, hata hivyo naiaminia management ya Rockstar4000 kv ni international.... labda Kiba mwenyewe ashindwe like Rose Mhando cjui alifika wapi na hii management manake kimyaaa kabisa!
 
Wanaomlaumu Diamond bado hawajui lack of education. Kama amethubuti kuongea mbele ys Rais kwamba yeye kuzaa na Zari ni maendeleo kwa Taifa hakuna atakalolifanya anishangaze.
Hicho unachosema majuzi Diamond nilimchana kwenye page yake alipotoa hoja ya kwamba "kwanini viongozi wote ni wa kabila lile lile...!" akihusisha CHADEMA na Wachaga! Mie sio shabiki wa UKAWA lakini nilikerwa sana na inaelekea wenye ufahamu walimwambia akafuta ile kauli lakini hata hivyo nilifahamu hapa tatizo ni elimu na uelewa! Mtu mwingine hata kama anaamini beyond reasonable doubt kwamba CHADEMA ni chama cha Wachaga lakini hawezi kuthubutu kuongea hadharani lakini kwa hawa wenzetu, ni ama waamue kupoga kimya kama afanyavyo Kiba au aongee na kuharibu kila wakati!
 
Domoo hana akili, kwanza nani atashawishiwa na domo afu akubali kuipigia ccm kura wakati at the first place alkua hataki? Mwacheni domo ajiharibie afu mwisho wa siku aje kusema "Watanzania wana chuki binafsi, wimbo wangu walikataa kuupigia kura kimataifa"
 
True kwa 99%... nimetoa 1% kwa sababu ulitakiwa kumalizia kabisa mwenye kipaji kikubwa ambae alibweteka na kipaji chake hadi alipokuja kukurupushwa usingizini! Leo hii Diamond anakuwa ndo wa kuonesha njia wakati alitakiwa kufuata njia ya wakongwe na talented kama Ali. Majority ya mashabiki wa Diamond walikuwa ni wa Ali Kiba. Anyway, hata hivyo naiaminia management ya Rockstar4000 kv ni international.... labda Kiba mwenyewe ashindwe like Rose Mhando cjui alifika wapi na hii management manake kimyaaa kabisa!
Nami nakubaliana nawe 99%....nimetoa 1% kwakuwa ulitakiwa kumalizia si tu kubweteka ila king walimstress watu flani wa media mpaka akaona ni bora nusu shari kuliko shari kamili....ila asikuambie mtu bongo kwenye huu mziki tunatisha africa!....huu ushindani wa kiba na diamond ukitoa fursa na wengine kutamba tutazidi kutisha!
 
Yaani am so excited ninapoona tunavyozidi kukimbiza... kwa mwendo huu, soon haitakuwa tena East Africa Giant ambayo tumeshaichakaza kila angle bali kote kusini mwa jangwa la sahara na kisha kumalizia umangani kaskazini mwa afrika!! Interest yangu kubwa kwa sasa ni kuona tunavuruga na kupiga show nyingi zaidi za Afrika kuliko za Marekani au US ambako kimsingi wanaokuwepo ni wana-East Afrika wenzetu tu na zaidi ya mkwanja, wala haisadii sana kueneza muziki wetu. Kwa sasa sidhani kama kuna music chat kubwa kwa Afrika kusini mwa jangwa la sahara ambako unaweza kukosa ngoma ya TZ!

Kuhusu ushindani wa Diamond na Kiba, ninaona una manufaa sana! Figisufigisu za hapa na pale haziepukiki... ikiwa hata makanisani na misikitini huwa zinakuwepo, seuze kwenye muziki !!!
 
of course yes i am a great thinker and genius as well too, domo ni public figure and is there for all fans regardless their political affiliations, to please and entertain the public as one is to not rely on any alliance.

mengi kazi yake ni kumake money kwenye media and politics is about media na sheria na maadili ya biashara yake yanamruhusu and mengi sio public figure he's just a business man anachotakiwa kufaanya ni kuwavutia wateja wake wanaompelekea hela kwa kutoa huduma bora za matangazo basi na wala hayupo close na jamii kama msanii ambaye yeye an deal na jamii direct and physically solely.

mengi ni company manager or member of the body of directors anaweza asiwe na umiliki wa kampuni ya IPP 100% bali ni kwa share fulani hivyo miradi yake haiendeshwi na yeye kama yeye kwa 100% and on top of that that is different business far from music, you got to know that.

Jitambue kaka msanii pia ni mfanyabiashara km mengi au dar express ...
 
Wewe uliyemwaga povu hapa unajidanganya...sawa wamefanya. Biashara na mipost ya shombo mayo wanalipwa uzalendo upon wapi?hao wamesahau wenzao wanaoteseka basi...hawataki ukombozi miaja 54 watoto kusomea kwenyed miti wkt kuka mahali Pesa za jumbo zinapelekwa?zinduka ---- wewe.
 
Would you mind if I opt to ignore you madam?!
 
Back
Top Bottom