Hapana, nadhani wanachofanya EFM ni kualika celebrity mmoja kila siku ili awe anasoma magazeti, siku ya kwanza baada ya kuondoka kitenge magazeti alisoma Elizabeth Michael, siku ya pili akisoma Shilole, siku ya tatu alisoma Kingwendu na siku ya nne kasoma Steve Nyerere.
Nadhani wanatafuta mtu ambae anaweza kutosha kwenye hicho kipindi, so kati ya hao ambao wanasoma seems ambae atasoma vizuri zaidi kuna uwezekano akala shavu kabisa.
Nilimsikiliza Kingwendu akiwa anasoma, aisee alikuwa anatetemeka kabisa, kuna muda mpaka Musa akawa anamsaidia kusoma.
Tusubiri Jumatatu tutaona nani ataalikwa kusoma magazeti.