Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Huu utaratibu wa watu kujichikuliia nyama wenyewe, ni watu 10-15 wamwanzo ndiyo watabeba nyama zote. Unakuta mtu amepanga nyama kama mlima Kilimanjaro.
Usiombe useme ladies first, wanaume hawatakuta kitu hao ladies ndiyo wataalamu wa kupanga milima ya nyama.
Hapa hata uwe umechinja kuku 50 na ng’ombe mmoja bado kuna watakao kosa nyama. Mchele si big deal ingawa unashushia nyama.
Kuna wanaokuja na mabakuli kwenye pochi, akichukua nyama anapunguzia kwenye bakuli ili na watoto nyumbani wapate.
Ukiweka caterers wagawa chakula kuna watakao rudia foleni mara tatu kwanza kabla hawajala.
Ustaarabu huku kwetu ni sinia watu wagawane nyama wenyewe. Kwenye sinia hakuna atakaebeba nyama atie kwenyebakuli.