Bill Lugano
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 1,189
- 6,450
Nimerudi siku chache zilizopita toka UK, nikaenda USA, nikapitia Canada, Egypt, China, Russia, Morocco na Saud Arabia kuna jamaa zangu walinialika kula sikukuu huko. Wadau hivi yale maziwa ya Camel mnawezaje kunywa? Mimi yalinishinda kabisa. Nyama yake huwa nakula mishkaki mara moja moja.
Leo nimekuja huku mnaita town, nimeshangaa magari hamna kabisa. Mpaka nikajiuliza kuna nini? au ndo mwisho wa Dunia umefika watu wenye maisha mazuri wanachukuliwa wakaishi Mbinguni? Lakini nikasema mmmh! Mi mbona bado nipo?" Naona tu Toyota, Subaru, Nissan .... vyombo vya usafiri. Lakini Range za miaka hii, Benzi, BMW , Ford ni nadra sana kuziona.
Nimejikuta nasimama pembeni ya Traffic kumuuliza kuna shida gani mbona naona tu usafiri unapita pita magari hamna.... akanishangaa na kuniuliza. "Boss kwani hujui mafuta yamepanda bei?" kwa kweli bila shaka yule traffic aliniona mimi mshamba sana. sikuwa hata najua kuwa mafuta yamepanda tena bei. maana jana nimejazilizia tena kwenye gari full tank. mi huwa nawaambia tu tank lijae. Nawauliza mnadai tsh ngapi nalipa, siulizi bei.
Kuuliza uliza bei ni ishara ya umaskini. mimi naulizia bidhaa kama ipo ikiwepo na nahitaji basi nachukua. siyo suala la kuuuliza bei. unauliza bei ili iweje? uliza kama mtu anauza kitu. Unamwambia akuletee kisha unamwuliza umpe tsh ngapi. mnafunga biashara.
Nimeambiwa wenye magari wengi wameacha magari home kwao wanatumia vyombo vya usafiri, but nimeshangaa tu mtu una miliki gari la milion 300 - 700 utashindwa kweli kununua mafuta lita moja tsh 5000? hapa unashindwa nini kutoa 400,000 ujaziwe mafuta au 500,000? tuachen roho za kimaskini.
Na Huu mchezo mtu anakukuta barabarani unaendesha gari halafu anakuovertake na usafiri wake wa Passo, Vits, IST sijui na nini nyingine kisha anakuja kufungua uzi huku JF kuwa usafiri wake unakimbia si sawa hata kidogo. Mimi naendesha sijui hata kama una nia ya kushindana nami. Wewe unajikimbiza mwenyewe kisha ukija JF unasema "jamaa alikuwa na Range yake nimemkata, alikuwa na BMW yake nimemkata Mikumi hakuniona tena.
Wewe unajikimbiza na Vitz, Subaru na sijui na nini. si sawa hata kidogo. ni kudhalilisha wenye magari. wakati mwingine najisikia uvivu kushindana na Toyota nini sijui mlizo nazo hapa kwenu. kweli mnataka Duma ashindane Mbio na Kondoo kuonesha Umahiri wake? Ni propaganda chafu za kutaka mwaribia jina Duma. Dunia nzima inajua anavyokimbia.
Mi nashauri tutafuteni pesa kuondoa hali ya malalamiko kila wakati. Ukiona gari za mafuta zinakusumbua nunua za umeme.