Uchaguzi 2020 Huku ni kuishiwa hoja za kisiasa na nidhahiri mgombea wa CHADEMA amejitanabaisha hafai kuwa Rais

Uchaguzi 2020 Huku ni kuishiwa hoja za kisiasa na nidhahiri mgombea wa CHADEMA amejitanabaisha hafai kuwa Rais

Sasa mnataka Lissu aongee nini maana huko kuropoka ropoka ndiko kulikompa umaarufu Lissu.
 
Pole sana kama unaendelea kumfuatilia huyu mtu.

Hafai hata kuwa mwenyekiti wa kijiji
 
Mimi binafsi nilitegemea kuwa Chadema mwaka huu baada ya kufanya makosa mwaka 2015 na kumsimamisha Lowasa kugombea urais,nilitarajia mwaka huu wangeweka mgombea makini na mwenye uwezo wa kunadi sera ambazo zinaweza kurudisha imani ya wananchi kwa chama hiki.

Lakini kadiri kasi ya upigaji kampeni inavyoongezeka inaonyesha wazi kuwa hali sio hivyo,maana kadiri siku zinavyokwenda ndio mgombea wao Tundu Lissu anazidi kuongea majukwaani hoja ambazo zinamuondolea sifa ya kuwa kiongozi wa aina yoyote kwa taifa letu. Maana mbunge,diwani hata mtendaji kata huwezi kuongea haya anayoongea Lissu.

Tundu Lissu ni mwanasheria na anajua kabisa Uhamiaji ni chombo ambacho kiliundwa kwa mujibu wa sheria za nchi yetu ili kudhibiti uingiaji na utokaji wa raia wa kigeni. Maana kama hiki chombo kisipokuwa makini hata usalama wa taifa letu unakuwa hatarini, maana wageni wanaoingia na kutoka sio wote wana nia njema kwa taifa letu. Kwa hiyo kusema hiki chombo kinahoji wananchi wa kigoma vyeti vyao vya kuzaliwa bila utaratibu ni kuongea pumba.

Kitendo cha Tundu Lissu kulalama majukwaani kuwa wananchi wa kigoma wamekuwa wakiulizwa vyeti vya kuzaliwa si cha kweli na hii ni uthibitisho kuwa amekosa hoja za kuibana serikali ili aweze kupata kura.
Ipo wazi Idara ya uhamiaji huwa wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria za nchi, na wanapokuwa na mashaka na uraia wa mgeni au mtu ambae hawana uhakika juu ya uraia wake lazima ahojiwe ili atoe inyaraka za kuthibitisha uraia wake. Na hili linafanyika kwa manufaa ya taifa kiusama na kisheria.

Hili halifanyiki kwa wananchi wa Kigoma tu bali linafanyika kwa Tanzania nzima iwe ni mikoa ya mipakani au hata isiyokuwa ya mipakani. Kwa hiyo kwa mkoa ambao upo mpakani kama kigoma,kwa manufaa ya taifa letu umakini ni lazima uwe juu zaidi.

Hoja kuwa wanaoikosoa serikali ndio wanahojiwa uraia wao, haina mashiko. Mimi nafikiri afahamu kuwa wengi ni wale ambao wanatokea maeneo ya mpakani ambao kwa namna moja au nyingine vyombo vya dola vinawahoji si kwa sababu ni wakosoaji, bali ni katika kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria. Kama hoja ni kuikosoa serikali basi hata marehemu Mch Mtikila angehojiwa uraia wake.

Kutamka hadharani kuwa eti rais Magufuli hana cheti cha kuzaliwa hii pia ni uthibitisho kuwa Lissu hana hoja za kuibana Ccm ili itoke madarakani.Lissu anayo access ya personal documents za JPM? mpaka aseme hana cheti cha kuzaliwa? Hii ni aibu kubwa sana kwa mwanasheria kuongea jambo kama hili hadharani,tena huku akitambua kuwa ni kosa maana hapo ni kama ameudanganya umma. Je kesho ikitokea cheti cha kuzaliwa cha JPM kikaonyeshwa hadharani atasema nini?

Chadema kama mngelikuwa nawashauri wazuri mngelikatisha kampeni za mgombea urais maana sasa ni kama kupoteza muda na pesa,huku mgombea wenu amekosa sera za kuambia atawafanyia nini watanzania na kubaki kuongea masuala yasiyo na msingi.
Kwa nini kila mkosoaji wa jiwe anaambiwa siyo raia wa Tz, afu anaombwa cheti cha kuzaliwa cha babu yake, bibi, mama, baba, na chake? Jiwe anavyo?
Mfano: Askofu Severine Niwemugizi, Askofu Kakobe, nk
 
Mbona unakosa Logic? YES kwa CCM ndiyo hivyo kama huna cheti siyo Mtanzania, si ndiyo nyie manawauliza mkiona wamewakosea???
Kama ana kiapo cha mahakama kinachothibitisha ni raia waTanzania, kinamuondolea kuwa raia wa Tanzania? Think twice!
 
Bashe na Kakobe walihojiwa kwa mujibu wa sheria kuhakiki uraia wao.

We pimbi usie na akili,Geita ni Burundi. Ndio unamshauri Lissu aropoke upuuzi?
Duniani hakuna siri huyo ni mrundi Mhutu , jitu limekuja limebebwa mgongoni kutoka uhutuni huko unafikiri watu hawajui , kwani Jiwe anaishi mbinguni ? Hana ndugu ? Hana jirani? Hana aliosoma nao ? Aliokuwa nao ? Wengine wamo humuhumu jf .
 
Duniani hakuna siri huyo ni mrundi Mhutu , jitu limekuja limebebwa mgongoni kutoka uhutuni huko unafikiri watu hawajui , kwani Jiwe anaishi mbinguni ? Hana ndugu ? Hana jirani? Hana aliosoma nao ? Aliokuwa nao ? Wengine wamo humuhumu jf .
Nonsense.
 
Back
Top Bottom