Huku Rwanda na Uganda wakizinguana, Kenya na Tanzania watunishiana misuli kwenye mpaka tena

Si mlianza na sisi tukamaliza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmesahau Kenya mlianza mienzi mitatu iliyopita acheni kulialia mlimwaga mboga tumemwaga ugali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmesahau Kenya mlianza mienzi mitatu iliyopita acheni kulialia mlimwaga mboga tumemwaga ugali.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii tit for that haijaanza Leo, ilianzia kitambo sana, kwahivyo ukisema Sisi ndo tulianza miezi mitatu iliopita ujue nyinyi ndo mlikua mmefanana kitu ndo tukaanza hivyo.... Usisahau wanabiashara wa Kenya Kwa mpaka wa namanga walikua wanaandamana miezi minne iliopita wakiitaka serekali ya Kenya ichukue hatua Kwa maovu yaliokua yanafanyiwa bidhaa zao hapo mpakani....
Nyinyi ndo mlianza na kutuchomea vifaranga vikiwa bado viko hai eti sababu vinaezakua na outbreak ya birdflue (ambayo Kenya haijawahi kua na outbreak hio) kwasababu hamjavikagua hivyo vifaranga... Na Sisi tukaregesha tit for tat, bidhaa zenu zote lazima tuzikague kama mara Tatu hivi sije zikawa na Ebola au magonjwa yoyote ambayo hayapatikani Tz, lazima tupime 'kila kitu'
 
Sisi sio tulianza hizi tit for that mlianza nyie mlipozuia Unga wa azam na gas hadi waziri wetu akawasiliana na waziri wenu lakini hamkusikia na sisi tukajibu tulishayazungumza yakaisha lakini mienzi mitatu iliyopita mkarudia tena. Hebu fikiria tumekuja kujibu mienzi mitatu baadaye jioni kama tuliwavumilia sana

Tatizo wakenya hamfualii viongozi wenu wanaifanyia nini tz lakini tukijibu mapigo nyie mnakuja kulialia humu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Which Kenya r u talking about? This same Kenya that bans Uganda's goods everyday!
 
He, kama utataka kujua haya yote yalianzia wapi, itabidi urudi zile nyakati za EAC 2.0 ilipoanzishwa tena na tukaamua kufunguliana mipaka, kwa miaka hio yote Kenya ilikua imefungulia mipaka TZ lakini Tz ilikua ikizulia baadhi ya makubaliano na kenya ilikua inanyamazia tu hio miaka yote....... kwa mfano Kenya ilikua ikiwachilia magari ya kitalii ya Tz kuingia mbuga za kenya wakati Tz ilikua inazulia, Kama Tz ilikua haitaki basi mngekataa wakati wa ku sign makubaliano, Lakini mlikubali alafu magari yakifika kwa mbuga yanakatazwa.... kuna wakati flani ilifika waendeshaji magari ya kiutalii walianza kuikosoa Serekali ya KEnya kwa kuruhusu magari ya TZ yaingie mbugani wakati ya Ke yalikua yanazuliwa huko TZ, Kenya ikaamua sasa pia sisi tutaanza na kukataza magari ya Utalii kutoka TZ kuingia JKIA kupokea wageni, Alafu TZ ilipoona hivyo ikapunguza safari za KQ kuingia TZ, baada ya hapo hio tit for tat ikaendelea hadi maziwa na sigara na bidhaa zengine ndogo ndogo ikafika wakati flani kukatulia, Alafu JPM alipoingia ndo hii tit for tat ikaanza tena, sasa hali imeeendelea kua mbaya zaidi.... Mlipotuchomea vifaranga hapo ndo mlivuka mpaka, Kenya na wakenya wote sasa wakaamua hatutasahau mlicho tufanyia..
 
Kwenye upande wa utalii sina kumbukumbu sana lakini kwenye upande wa bidhaa nyie ndo mlianzisha hasa kwenye Unga na gas.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye upande wa utalii sina kumbukumbu sana lakini kwenye upande wa bidhaa nyie ndo mlianzisha hasa kwenye Unga na gas.


Sent using Jamii Forums mobile app
Wala usisikilize kelele na Maneno mengi ya hao Wakenya, Hawa ni wabinafsi sana wanataka kila kitu wafaidike wao, walishindwa kufanya kazi na Nyerere mtu asiye na ubinafsi hata kidogo, mtu mwenye kuwapenda watu wengine zaidi ya anavyojipenda yeye mwenyewe, watawezaje kuishi na watu wengine?, Hawa ni watu wa kulialia tu ili waonekane ni watu wema wakati ni watu katili, wabinafsi na wabaguzi sana, kiboko yao ni uncle Magu, aendelee kuwanyorosha hadi wabadilike.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kati ya Original EAC members, Uganda (Nchi yenye uchumi mdogo kuliko Tz) inauzia Kenya bidhaa zenye thamani ya millioni $640 million wakati Tz inauzia Kenya bidhaa hazifiki hata nusu ya hio... Kati ha hizo nchi zote Uganda inapakana nazo, Tz ndo inauziwa bidhaa chache zaidi, hio graph inaonyesha ni nani ndo ana ubinafsi mwingi zaidi na majirani wake... Wa tz kwa maneno hamna mpinzani lakini kwa vitendo zero kabisa...

 
Baada ya EAC kuvunjika mwaka 1977, Nyerere alipoteza imani na Kenyatta na Idd Amin, aliamua kugeukia nchi za kusini mwa Africa na kuanzisha vuguvugu la kuanzishwa kwa SADC, tameona faida na umuhimu wa kufanya biashara na SADC kuliko na EAC, kule tunaishi kama ndugu wa baba na mama mmoja, hakuna mivutano ya kijinga.

Mwaka Jana pekee balance of trade ya Tanzania na nchi za SADC ilikua $445M, wakati na EAC ilikua only $130M, unategemea tutapendelea EAC ambako mivutano ya nchi kwa nchi inaendelea kila siku?.

SADC kuna 16 member states, hakuna Vita Wala migogoro baina ya wanachama, EAC kuna nchi sita, lakini
1)Rwanda na Burundi hawapatani
2)Rwanda na Uganda hawaelewani
3)Uganda na Kenya wanagombea Migingo
4)Kenya na South Sudan wanagombea "the so called triangle"
5)Kenya na TZ misuguano ya biashara haiishi

Hivi kweli unategemea Tanzania iwe serious kufanya biashara na nchi za EAC?, Kenya na Uganda Hamna alternatives, that's why you must concentrate among EAC.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kenya na Uganda zingekua hazisikizani tungekua hatufanyi biashara period! hakuna cha sijui hakuna altanetives wala nini, Alafu ukumbuke biashara inafanywa na wanabiashara sio serekali, wanabiashara ndo huamua ni wapi watauza bidhaa zao, Kwahivyo serekali yenu ikiamua kufungulia mipaka Kenya wanabiashara wa Tz wataweza kuuza bidhaa zao Kenya kwa wingi sawa sawa na wakenya wataweza kuuza bidhaa zao nyingi huko Tz...... Kabla hii migogoro yote ianze Tz ilikua iki export zaidi ya $350m to kenya...
Kule SADC hua mmetulia manake hamna nguvu za kutunisha misuli na kina SA, alafu nchi za SADC ni nyingi si kama EAC nchi tano pekee na mbili ni sawa na mkoa ) lakini usijidai eti hakuna migogoro huko SADC ,
1)Tanzania na Malawi Lake nyasa Dispute
2) Zambia -Malawi border demarcation dispute
3)Angola and Congo are always accusing each other of something
4) CAR and DRC are always fighting over water resources at the border
5) Zimbabwe Botswana border disute in Kazungula frontier

Upende usipende, despite problems EAC is the most integrated economic block on the Continent! Tz ndo inaturegesha nyuma ingekua tulifika mbali sana.... East Africa trading bloc ranked high in regional integration : The Standard
 
Sasa Mbona unalazimisha mambo?, nimekuambia Tanzania biashara tunayoifanya SADC ni mara tatu ya ile tunayoifanya EAC, lazima tuthamini zaidi SADC kuliko EAC.

Kuhusu migogoro ndani ya SADC, yote inasuluhishwa ndani ya SADC, kwasababu tunaishi kama ndugu, hujawahi kuvuka hatua ya kushutumiana nchi moja kutaka kupindua nchi nyingine kama ilivyo Burundi na Rwanda au Rwanda na Uganda.

Ukiacha Malawi na Tanzania, hakuna mgogoro mwengine wowote ndani ya SADC unaohusisha mipaka, Wewe ni mwongo mkubwa sana. Angola na DRC hawana ugomvi. CAR haipo SADC Ndio sababu sijataja Kenya na Somalia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui kama sijaelewa vizuri,issue ni mgogoro wa mipaka au ni kutokuwa na uhakika kama bidhaa zimetimiza vigezo vya ubora vya nchi husika na ndio maana mamlaka za nchi husika zikataka kujiridhisha??
 
Sijui kama sijaelewa vizuri,issue ni mgogoro wa mipaka au ni kutokuwa na uhakika kama bidhaa zimetimiza vigezo vya ubora vya nchi husika na ndio maana mamlaka za nchi husika zikataka kujiridhisha??

Mambo mengi tu, yaani kwa kifupi huu muungano ni jina tu na chochote chaweza kutokea tukauvunja.
Kumbuka Tanzania juzi ilikua inawazingua Waganda kwenye sukari yao. Hiyo hiyo Tanzania iliwabania Wazanzibari kwa hilo hilo la sukari.
 
kenyans are always snitcher
 

wakenya kwa kifupi hamtuwezi, mlijaribu kidogo sana wakati tukiwa buzy na ukombozi wa kusini mwa bara la afrika sasa tuna nafasi na muda wa kutosha wa kupambana na walaghai wa kibiashara na uchumi kama nyie STAY ON
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…