Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Baada ya kilio cha muda mrefu na kutegeana kwa mataifa ya magharibi yanayoisaidia Ukraine kupambana na Urusi hatimae mataifa hayo yamekubali kuipelekea Ukraine ilichodai kwa muda mrefu navyo ni vifari vya Leopard kutoka Ujerumani na Abrahms kutoka Marekani.
Hata hivyo muda mfupi baada ya kuahidiwa silaha hizo raisi huyo wa Ukraine aliyewahi kuwa muigizaji mahiri amesema kinachotakiwa hasa ni ndege za kisada za kivita kutoka mataifa hayo na makombora ya masafa marefu kuliko HIMARS.
Kauli hiyo imekuja wakati pia nchi hiyo imetoa tamko rasmi la kuondoa askari wake kutoka Soledar ambako jeshi hilo lililshindea kuudhibiti mji huo baada ya kipigo cha Urusi jambo ambalo pia Ukraine ililikanusha mara kadhaa baada ya tangazo la Urusi.
Wakati huo huo aliyekuwa waziri mkuu wa Japan bw.Mori ameishutumu nchi yake kwa kutoa umuhimu mkubwa wa kuisadia Ukraine katika vita vyake ambavyo alisema wala Urusi haiwezi kushindwa kamwe katika vita hivyo.