Huku wakiondoka 'Kisifasifa' na 'Kishamba' kwenda Kigali Wapinzani wao Wamepandisha Bei za Tiketi na sasa Kiingilio ni Laki Moja za Tanzania

Huku wakiondoka 'Kisifasifa' na 'Kishamba' kwenda Kigali Wapinzani wao Wamepandisha Bei za Tiketi na sasa Kiingilio ni Laki Moja za Tanzania

Mkiambiwa Mpira wa Afrika ni Vita na kutokana na Ugeni wenu jifunzenj kutoka kwa Wazoefu wa Mashindano ya Kimataifa Simba SC hamtaki.

Taarifa ikufikie kuwa kuna Tetesi kuwa Klabu ya El Merreikh ya Sudan imepanga Kuongeza Bei ya Tiketi kwa Mashabiki kuingia Siku ya Jumamosi.

Wakati Mashabiki wa Safiri Kigali Kisifasifa na Kishamba FC wakiwa Wameshazoea kuingia kwa Buku ( Tsh 3,000/= ) Tatu au Kuingia Bure ( Fungulia Mbwa ) Uwanja wa Benjamin Mkapa hivi sasa kama Shirikisho la Soka Rwanda na CAF hawatoingilia Kati basi kila Shabiki atalazimika kulipia Shilingi Laki Moja ( Tsh 100,000/= ) kwa Tiketi.

Kwa jinsi GENTAMYCINE ninavyowajua Mashabiki wa Timu hiyo walivyo Masikini ( Choka Mbaya ) Kifedha na Kimaisha pia upo Uwezekano 99% yao wasiweze Kuingia Uwanjani ( Pele Stadium ) kuangalia Mechi yao na wakabakia katika Mabasi yao wakimsikiliza Hassan Mvula akiutangaza Redioni na Wengine wenye Simu wakiangalia huko huku Wengine Wakiwadoea Kuangalia na Midomo yao ikipiga tu Miayo kwa Njaa Kali.

Taarifa kuwa Klabu ya El Merreikh ya Sudan imepanga kufanya Umafia huu ( ambao GENTAMYCINE nimeubariki na naupenda ) imeripotiwa muda si mrefu katika Kipindi cha Sports Bundle cha 107.3Mhz UFM ( Azam Media ) muda si mrefu na Mimi ni Mjumbe tu hivyo kama kuna Mtu ataichukia basi awakasirikie Wao ( Walioileta ) na siyo Mimi.

Safi sana El Merreikh FC mmenjfurahisha.
Muda wote wewe ni mtu wa kunawashwa washwa tu.
 
Uzuri wa wachezaji wa Yanga ya sasa huwa hata hawajui kama uwanjani kuna mashabiki au hawapo
 
Ukitaka kuficha madhaifu yako basi jiepushe kuwa muongeaji sana. Binafsi huyu GENTAMYCINE nimegundua ni jamaa fulani lofa sana NA HOJA ZAKE NYINGI HUWA HAZINA MANTIKI. PIA ANAONEKANA NI MTU MWENYE STRESS SANA KATIKA NDOA YAKE
 
Ukitaka kuficha madhaifu yako basi jiepushe kuwa muongeaji sana. Binafsi huyu GENTAMYCINE ni jamaa fulani lofa sana NA HOJA ZAKE NYINGI HUWA HAZINA MANTIKI. PIA ANAONEKANA NI MTU MWENYE STRESS SANA KATIKA NDOA YAKE
Ila huyu Jamaa hachelewi kukuchongea upigwe ban
 
Back
Top Bottom