pingli-nywee
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 11,923
- 13,350
Kama kawa kama dawa. Wanariadha wa Kenya wameng'aa kule London Stadium, U.K., kwenye mchuano wa IAAF 10th Leg Diamond League 2019. Hii ni baada ya wakenya kunyakua nafasi 8 kwenye top 10 ya mbio za 5,000m kwa kina dada.
Helen Obiri alinyakua nafasi ya kwanza akifatwa kwa karibu na Agnes Tirop(2) kisha Margaret Kipkemboi(4). Alafu Caroline Kipkirui(5), Cherono(6), Chebet(7), Rengeruk(8), na Kite(9).
Yaani ilikuwa ni mwendo wa; [emoji1139][emoji1139][emoji1139][emoji1139][emoji1139][emoji1139][emoji1139][emoji1139]. Wanaume nao hawakuachwa nyuma, siku ya kwanza ya mchuano huo walifanya yao pia. Kwenye mbio za 800m.
Ferguson Rotich alishikilia nafasi ya kwanza na Wyclife Kinyamal akawa wa pili. Kenya hoyeeeee!!!