Hukumu imetolewa bila kuzingatia ushahidi uliotolewa

Mpindo

Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
62
Reaction score
54
Wakuu,
Nilikuwa na kesi ambayo ilikuwa tunagombea kipande cha Ardhi. Ushahidi pande zote ulitolewa, mimi nilikuwa mlalamikaji. Hukumu ilitolewa kwamba mimi sina haki. Lakini katika mwenendo wa kesi baada ya kufuatilia ilibainika Hakimu hakuwa anandika ushahidi uliokuwa unatolewa wa kwangu na mashahidi wangu ule mzuri ambao ulionyesha eneo lile lilikuwa langu. Sasa katika mazingira hayo nitalalmikaje? Na kwa nani? Kwa sababu ukisoma hukumu na mwenendo wa kesi ni kama mimi sikiwa na mashahidi, kwamba hata mashahid wangu eti wamenikataa, wakati ukweli ni kwamba mashahidi wangu walitoa ushidi wa kuunga mkono kwamba mimi ni mwenye haki.

Naomba mniambie nafanyaje kwasababu hakimu alivyoamua ni kama alikuwa na upande wake tayari hata kabla ya Hukumu.
 
Mmmh mkuu pole sana...hapo kuna mchezo umechezewa nahisi..Tafuta wakili mzoefu akupe ushauri mzuri
 
Pole Mkuu , namimi umenipa mwanga na kunishitua, kunashauri kama lako na ninahisi hukumu ishapangwa kabla ya kesi kuisha.....!!! Mahakama zetu hizi za ovyo kabisa
 
Kwanza je kesi ilikuwa baraza ama mahakamani?. Pili kufanya hyo ni kukeukwa kwa maadili ya utoaji haki.

Maana kesi za Ardhi (Land dispute) husikilizwa na barazala kata, baraza la Ardhi na nyumba la wilaya, na mahakama kuu.

USHAURI
1. Kata rufaa kupiga tunuku hyo.
2. Peleka malalamiko yko kwny mamlaka za kinidhamu za chombo husika kilichofanya hicho kitendo
2.1 kama ni baraza la kata (WT) peleka malalamiko yko kwa mkurugenzimyendaji wa H/W ambalo baraza lipo.
2.2 kama ni baraza la Ardhi na nyumba la wilaya (DLHT) peleka malalamiko yko wizara ya Ardhi.
2.3 kma ni mahakama kuu peleka malalamiko yako tume ya utumishi wa mahakama ama wasiliana kwa whatsApp na uongozi wa mahakama ya TZ namba 0752 500 400.
 
.
Umejibu vyema. Akifuata hatua hizo hakika haki yake kama ipo itapatikana.
 
Ahsante mkuu kwa ushauri,
Lilikuwa Balaza la wilaya la Ardhi.
Je! Nikipeleka malalamiko wizara ya Ardhi na hukumu imetoka watarekebisha maamuzi!
Kesi itaweza kusikilizwa upya au ndio wataendelea na taratibu za kinidhamu tu?
 
Ahsante mkuu kwa ushauri,
Lilikuwa Balaza la wilaya la Ardhi.
Je! Nikipeleka malalamiko wizara ya Ardhi na hukumu imetoka watarekebisha maamuzi!
Kesi itaweza kusikilizwa upya au ndio wataendelea na taratibu za kinidhamu tu?
Wataendelea na taratib za kinidham tu dhidi ya huyu mwenyekiti wa DLHT. Halaf haki itatendeka kwa kukata rufaa HCT ambapo mahakama (HCT) ndo itaelekeza kama ni kuisikiliza kesi (trial) ama kuirdisha DLHT kusikilizwa upya (trial denovo)

NB; Neno "haki itatendeka" simanishi wewe ndo utashinda haki kutendeka means kufuatwa utaratibu wa kisheria kwa mujib wa sheria husika. Hata km ukishinda ama ukashindwa lkn kwa misingi na kanuni za utoaji haki basi hapo kisheria haki imetendeka.
 
Wewe mrembo Upo vizuri...
You deserve my hug!!
 
Kwakuwa shauri lako lilikuwa DLHT nakushauri kata rufaa High Court ( LAND DIVISION) wataipima hiyo haki.Pia naunga mkono ushauri uliotolewa na Dragoon.
 
Ahsante mkuu,
Nitafuata ushauri huo.
 
Njoo kwa Babu huku Matombo, ana Dawa yao wazulumati kama hao.
 
Njoo kwa Babu huku Matombo, ana Dawa yao wazulumati kama hao.
He!
Mkuu sasa huyo Babu anafanyaje, make watu wa jinsi ya hakimu kama huyo ni kuwashusha mishipa! Teh teh teh!
 
Pole sana kwa kadhia hiyo

Cha msingi ni kukata rufaa katika mahakama ya juu zaidi ya hiyo iliyotoa uamuzi...mahakama ya kwanza kusikiliza rufaa inaruhusiwa kusikiliza ushahidi kwa hiyo unaweza kutoa ushahidi wako ulioachwa kuandikwa katika mahakama hiyo uliyokata rufaa..
Lakini pia usiache kuripoti kiutawala juu ya mtoa uamuzi huyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…