Mwanaukweli
JF-Expert Member
- May 18, 2007
- 4,786
- 1,715
kwani alihukumiwa miaka mingapi?
Nimeangalia katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nimekuta haya:
Ibara ya 67
(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge-
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu.
Nisaidieni tafsiri ya kifungu hicho.
Faini na kifungo viko at per ! lakini wanasheria ndio wanacheza hapo, kwani sheria iko kimya kama mtu amelipa faini!
Katiba haisemi kosa la jinai bali kosa lolote lile,
Nanukuu tena
Ibara ya 67
(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge-
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu.
Nisaidieni tafsiri ya kifungu hicho.
Kuamua kulipa faini haifuti kuwa amehukumiwa kufungwa kwa zaidi ya miezi sita.
Hapa kunahitaji wanasheria kuja kutupa tafsiri halali ya kifungu hicho
Kumbuka kwamba hiyo ni traffic offence ina tofauti na kesi zingine za jinai.
Usichanganye kati ya Ukiwaona Ditopile Mzuzuri (RIP) na Chrisant Majiyatanga Mzindakaya. Rudi hapa umuombe radhi Dr. Mzindakaya, alifanya kazi kubwa pale Sumbawanga kuhakikisha msimamizi wa uchaguzi anamtangaza mgombea wa CHADEMA kuwa mshindi kama wapiga kura walivyoamua, lakini akazidiwa nguvu na Pinda aliyetumia uwaziri mkuu wake. Ilikuwa kama sinema ya kuigiza kumuona Mzindakaya anatetea haki ya wana CHADEMA, hali iliyosababisha vigogo hao washikane mashati!Malipo ni hapa hapa duniani, Ditopile Majiyatanga Mzuri yupo wapi? kifo cha aibu kilimkumba. Labda Chenge atubu na kumrudia muumba vinginevyo duh.
Wanajamvi,
Kesi ya Chenge ndio imekwisha. Amekutwa na hatia na amehukumiwa hukumu ambayo sipendi kusema chochote hapa.
Ninavyofahamu mimi, mtu aliyewahi kutiwa hatiani na mahakama kwenye makosa ya jinai, anapoteza sifa ya kuwa kiongozi wa nafasi kama ya Ubunge (kama nimekosea nisahihisheni)
Sasa, hatima ya Chenge ni nini? Au kulindana kutaendelea?.