Hukumu ya kifo ya mwalimu aliyemuua mwanafunzi kwa kiswahili

Nimelia aisee
 
Daaaah nimeisoma kwa makini hii kesi. Ukweli ni kwamba matukio kama haya ni mengi sana mashuleni. Wanafunzi wanapitia mateso na manyanyaso mengi sana wakiwa shule.

Miaka hiyo wakati nasoma shule ya msingi kuna jamaa yetu alipigwa kwanzia tupo assembly (tulikuwa tukiita mstarini) hadi muda wa mapumziko, huku akiwa amefungwa kamba na anamwagiwa maji. Hakuna mwalimu aliyeingilia kati kwamba adhabu inatosha.

Kisa alipita njia ambayo ipo karibu na bafu la mwalimu (kwenye nyumba za shule). Kuna mwalimu alikuwa anaoga. Mwalimu akajasema jamaa alikuwa anamchungulia, kesi ikaenda kwa mwamba huyo sijui ndo alikuwa anamla. Kesi ikabadilika ikawa alitaka ambake mwalimu. Jamaa alipigwa hadi tukahisi anakufa
 
Maskini Mwanafunzi alipitia mateso kama ya Yesu kristu mwana wa Nazareth. Kifo chake kilikuwa cha mateso Mno. Mwalimu hakuwa na Huruma maskini
Nukuu ya kesi
"....…...Mwalimu Respicius akaendelea kumpiga Sperius huku akisema “huu ni usanii, hivi sivyo wanavyozimiaga”*
Wakasimama pale kwa muda. Sperius akapata nguvu. Akasema kwamba hawezi kutembea na akaomba kubebwa
Mwalimu Respicius akampiga tena akisema huo ulikuwa ni “usanii” kama mpango (plan) wa kutoroka. Akaagiza Wanafunzi wavue masweta yao Kisha wampepee apate hewa. Wanafunzi wakafanya hivyo.
Sperius akapata nguvu kiasi. Wakaelekea jengo la chekechea kutafuta pochi. Lakini hawakuweza kuipata. Mwalimu Respicius akampiga kichwani. Sperius akaanguka chini. Akapiga kifua kwenye jiwe. Akaishiwa nguvu.....
""
Hakika ulikuwa mwisho mbaya Sana kwa Mwanafunzi Sperius

Pumzika Salama Mtoto. Sisi sote tutakufa ilitakiwa wote wapate Adhabu ya jela
 
Mkuu, kwenye mikesi mikubwa mikubwa kama hiyo ya mauaji, wanaangalia je muuaji aliua kweli, je ni yeye, alidhamiria kuua?

Vipengele hivyo vya dodoso ndiyo mwishoni huamua kutofautisha adhabu iwe kuachiliwa huru, manslaughter au mader.

Hawaangalii sababu nyingine hapo, ndiyo maana huyo mwalimu aliyeanzisha sekeseke akatemwa.
 
Jaji katoa hukumu ya haki.

Hatujui sasa mbele ya safari, jamaa kama hakuridhishwa na hukumu, kama alikata rufaa na rufaa yake hiyo kutupiliwa mbali ama kukaziwa hukumu, hatuelewi nini kilifuata.
 
Aisiii!
 
Kuna Binaadamu ni makatili sana,na lazima watakua ni wakala wa Shetani!!
 
Mmmmmhhhhhhhhhhh...
Kujua sheria nimuhimu sanaaa.., nimejifunza vitu vingi sana. Shukrani kwa ku post JF
 
Nasikia alikata rufaa na kutoka jela mwezi aguast mwaka huu!!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…