Hukumu ya Mawakili wa Lissu kutolewa leo tarehe 16 October

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma inayoketi jijini Dar es Salaam, leo Ijumaa inatarajiwa kutoa hukumu katika shauri la Kikatiba Na. 7300/2026 linalohusu haki za faragha na fursa ya kuonana kati ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, na mawakili wake.

Vigogo na makada wa CHADEMA wakiwemo Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Dkt. Rugemeleza Nshala, na Wakili Paul Kisabo wamewasili katika Ukumbi Namba 01 wa Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam wakiwa karibu na Tundu Lissu kushuhudia utoaji wa uamuzi huo wa kihistoria.

Shauri hilo lilifunguliwa na Mawakili Maduhu William na wenzake wawili dhidi ya Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP), Mkuu wa Gereza la Ukonga, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), huku Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kikishiriki kama mdaawa mwenye maslahi.

Waleta maombi hao wanahoji na kupinga kitendo cha Maafisa wa Magereza kuingilia faragha ya mawasiliano kati ya mawakili na mteja wao kwa kusikiliza mashauriano yao, pamoja na kuwawekea vizingiti vya kuonana na Lissu, aliyepo mahabusu akikabiliwa na kesi ya uhaini isiyo na dhamana.

Jopo la Majaji watatu linaloongozwa na Jaji Amir Mruma, akisaidiwa na Jaji Dkt. Angelo Rumisha na Jaji Dkt. Evaristo Longopa, linatarajiwa kutoa majibu ya kikatiba kuhusu:
1. Iwapo Maafisa wa Magereza kusikiliza mashauriano ya mawakili na wateja wao ni kinyume cha Katiba.
2. Iwapo kuwawekea vizingiti mawakili kuonana na wateja wao magerezani ni ukiukwaji wa haki za kikatiba.
 
ok. 🐒
 
Mtihani mkubwa Mahakama leo. Let wait and see.

My take: Sioni mwenye uthubutu!
 
Tanzania tuna hitaji katiba mpya kuliko tunavyo dhani.

Hivi kesi ya Lisu hukumu yake ni mwezi ujao.

Huyu mtu alifungua shauri tangu mwanzo Akiomba Aki yake ya kuwasiliana na wanasheria wake kwa uhuru.

Mkamnyima Alafu Leo mnakuja kujidai mnatoa hukumu Ambayo haita msaidia tena mshtakiwa.

Sasa ya Nini basi? Utagundua mihimili hii bila katiba mpya haziko huru.
 
Magereza ukonga Wameshindwa kesi:
 
Attachments

  • IMG_6633.jpeg
    IMG_6633.jpeg
    227.4 KB · Views: 10
Tanzania tuna hitaji katiba mpya kuliko tunavyo dhani.

Hivi kesi ya Lisu hukumu yake ni mwezi ujao.

Huyu mtu alifungua shauri tangu mwanzo Akiomba Aki yake ya kuwasiliana na wanasheria wake kwa uhuru.

Mkamnyima Alafu Leo mnakuja kujidai mnatoa hukumu Ambayo haita msaidia tena mshtakiwa.

Sasa ya Nini basi? Utagundua mihimili hii bila katiba mpya haziko huru.
Ni sahihi, hii AMRI imechelewa , bila shaka, hii hali ya kutokuonana na Mawakili wake kwa faragha ilimuathiri Mh Lissu wakati wa kuandaa utetezi wake..lakini itasaidia kuweka kile wazungu wanaita "Precedent", kwa Wahaini na watuhumiwa wengine watarajiwa..Uzuri wa Mh Lissu na wanasheria wao huwa wanaona mbali
 
Huyo mkuu wa gereza afungwe gereza hilo hilo la ukonga ajifunze pimbi huyo!
 
Back
Top Bottom