Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duuu hii inatakiwa ikemewe na kumsaidia huyu mtoto kwa kweli.....JF pse naomba tuungane kwa uwezo wetu tumsaidie huyu mtoto kwa kwelii maana sidhani kama hakukuwa na option zaidi kifungoo......hapana sio kiihivyoo...atakosa haki zake kimsingi......kama shule hata future yake itaharibika pia umri wake haikupaswa kutiwa hatiani hapa kuna mazingira ya rushwa lazima......wanaharakatii...psee
hii ni hukumu iliyotolewa na mahakama uko wilaya ya bunda na kumtia hatiani mtoto huyu wa miaka 13 na kuhukumiwa kwenda jela miaka mitano (5). Kwa kosa la kunywesha mifugo maji kwenye mto rubana. Jamani ebu tujadili uhalali wa hukumu hii hata kama vifungu vya sheria vinasema hivyo lakini na busara pia inakiwa itumiwe na mahakimu wetu kwa kuangalia mazingira ya kosa na umri wa mkosaji pia. Mimi nafikiri taasisi za kutetea haki pamoja na wanajamii wote tunatakiwa kulizungumzia hili kwa kina ili kuweza kuwaweka sawa mahakimu wetu.
tanzania ilikufa na nyerere wake.
Nchi hii si mali ya wazalendo tena, ni ya wageni.
Je wewe hujasikia maamuzi dhidi ya wale waarabu watatu wa rujewa mbalali mbeya, laiompiga mtoto wa shule na kumuua kwa kosa la kuiba mapera????
Leo tunaambiwa eti amekufa baada ya kujirusha kwenye gari,
lakini taarifa za awali zilisema kuwa mtoto alipigwa hadi kufa...
Mi yangu mamcho.
Huu ni uonevu wa hali ya juu. Kwanza kimaisha mtoto huyu ameshayaumba tayari kwa kuwa elimu tena hakuna, kama hakumaliza darasa la saba then atasomaje secondary?? Au akitoka jela atakuja kusoma MEMKWA??? Na hata kama atapata nafasi ya kusoma hiyo elimu ya ngumbaro unataka kuniambia atasoma kweli wakati akiwa jela for sure anapata elimu dunia ya kumpatia short cut za maisha?? Ni wakati sasa umekuja tuwe na dedicated community Lawyers.
Nafikiri nahitaji kwenda kusoma sheria sasa, nibadili proffession totally na nijikite fully katika advocate wa community causes. Nina amini nikiandika proposal kwa ajili hii na nikiji commit kabisa bila tamaa nitapata wafadhili na nitafungua law firm kubwa sana na ya maana kuliko za sasa za biashara tu bila kujali haki. Inaniuma sana kama mzazi.
nakumbuka maneno ya dr sengondo,m aliyasema akihojiwa na mwandishi kuwa mawakili na wasomi wako busy kuwatetea matajiri na watu wakubwa na kuwasahau walalahoi na masikini wa_tz. Jamani hivi hakuna mawakili wa kumtetea huyu mtoto,mko wapi ngo's, mko wapi tawla,nemc, mama ananilea nkya na team yake ?
Nashindwa kuelewa upeo wa hakimu na baraza lake waliotoa hukumu hiyo, ni wazazi kweli,je ni kiasi gani maji hayo yameharibiwa na hao mifugo ukilinganisha na yale ya mto(nimesahau jinale) yaliyoharibiwa na mgodi wa north mara na kusababisha mifugo kufa na majani kukauka? Je kama ni hukumu mgodi huo utafungiwa miaka mingapi?.
Jamani sijui sheria wala sijasomea, lakini kwa upeo nilionao hukumu mara nyingi inalenga mafundisho, sasa haya ni mafundisho au kumkomoa mzazi? Nini matarajio ya kijana akitoka jela? Je kijana akitoka jela na kusikia au kuona kuwa north mara-mgodi bado wanaathiri mazingira na maji ya mto bila kuchukuliwa hatua atakuwa amejifunza nini.
Ingelikuwa rwanda, watu wangeliuliza hakimu alikuwa kabila gani? Je sisi hapa tz tuseme nini kama sio ufisadi.
Naitazama hukumu hii kama fundisho kwa wazazi wanaoweza kuwatumia watoto wao kuvunja sheria. Tukiacha watoto wafanye wanavyotaka, heunda hata 'mtoto' wa miaka 18 akatumwa kufanya 'maajabu' zaidi, Je, tutegemee wanaharakati wa haki za binadamu kutetea uvunjaji wa sheria?