hukumu ya mwanamke aliemsingizia baba mtoto

deborahk

New Member
Joined
Jun 26, 2012
Posts
3
Reaction score
0
hivi kama ikitokea ukisingiziwa mtoto na mwanamke halafu ukamlea, kumsomesha na kumpa kila kitu kwa kujua huyu ni mwanao, ikaja siku mtoto amekuwa yuko chuo kikuu anajitokeza mtu ambae ni baba ake biological (kwa ushahidi wa DNA) na anamtaka mwanae...je hamna sheria yoyote inayokulinda wewe uliemlea au hamna sheria yoyote inayomhukumu yule mama aliekusingizia...kiufupi nini kitakulinda wewe au hukumu gani itatolewa kwa yule mama aliekusingizia...na je gharama zako zinaweza kurudishwa, zile za shule na chakula na mengineyo?
 
Nadhani inawezekana ukapata haki yako, wafungulie kesi ya madai huyo mwanamke na huyo baba wa mtoto.
 
Wapo watu kibao wanaolea na kusomesha watoto ambao siyo wao,
Wewe si ulifanya kwa hiari mkuu.
 
sio kwahiari kaka ndio maana ya kusema neno kusingiziwa maana yake hukujuwa ukweli, ni mke umemuoa halaf mkazaa mtoto then imetokea hivyo sasa unafanyaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…