hivi kama ikitokea ukisingiziwa mtoto na mwanamke halafu ukamlea, kumsomesha na kumpa kila kitu kwa kujua huyu ni mwanao, ikaja siku mtoto amekuwa yuko chuo kikuu anajitokeza mtu ambae ni baba ake biological (kwa ushahidi wa DNA) na anamtaka mwanae...je hamna sheria yoyote inayokulinda wewe uliemlea au hamna sheria yoyote inayomhukumu yule mama aliekusingizia...kiufupi nini kitakulinda wewe au hukumu gani itatolewa kwa yule mama aliekusingizia...na je gharama zako zinaweza kurudishwa, zile za shule na chakula na mengineyo?