TTCL na mashirika mengine ya Serikali ni aibu kubwa kwa taifa hasa kwa wanayoyaongoza mashirika hayo, uzembe ni wa kiwango cha hali ya juu imefikia mpaka wafanyakazi kutojali tena pindi mteja utakapo huduma utasikia unaambiwa sasa mimi nifanyaje? Nilifika TTCL Kijitonyama kutaka kujua taratibu za kuunganishwa fiber internet nyumbani wakanipatia fomu na kuambiwa huduma zangu ntapata ofisi zao zilizopo Tegeta Kibo Complex, kufika pale naambiwa yanipasa kusubiri kwa muda wa miezi 2 mapka 3 nilistaajabu Saną huyo dada akaniambia kama unaharaka sana nenda kampuni nyingine bila hata aibu. Kwa mwendo huo hakuna shirika la serikali linaweza kufanya biashara kwa ufanisi na likatengeneza faida mkaguzi na mdhibiti wa Serikali ataendelea kuja na ripoti zenye madudu kila mwaka na bungeni watapiga siasa mambo yatapita huku Nchi ikiendelea kutafunwa na Wenye meno.