DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Hukumu ya shauri la Liston Katabazi dhidi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyokuwa itolewe tarehe ya hukumu ya shauri hilo Aprili 23, 2025 katika Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam imeahirishwa Juni 16, 2025.
Rufaa hiyo ilikuwa isikilizwe na Jaji Butamo Philip, imeahirishwa kwa sababu Jaji kuwa nje kikazi huku Katabazi na Wakili wa TFF, Rahim Shaban wakihudhuria mahakamani hapo.
Hivi karibuni Mahakama Kuu, ilielekeza rufaa ya Kocha Liston Katabazi aliyoikata dhidi ya TFF, akipinga uamuzi Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, isikilizwe kwa njia ya maandishi.
Rufaa hiyo ilipangwa kusikilizwa na jaji Butamo kwa mdomo, Alhamis, Machi 20, 2025. Hata hivyo Jaji Butamo alielekeza rufaa hiyo isikilizwe kwa njia ya maandishi.
Hivyo, alielekeza mrufani, Katabazi anayewakilishwa na mawakili Peter Majanjara na Melchzedeck Joachim kuwasilisha hoja zao za maandishi Aprili 2, 2025 na wajibu rufani kuwasilisha majibu yao ya hoja za mrufani, Aprili 16, 2025, mambo ambayo yametekelezwa.
Pia alielekeza kama mrufani atakuwa na majibu ya nyongeza dhidi ya majibu ya wajibu rufani yawasilishwe mahakamani Aprili 22 na kwamba rufaa hiyo ilitajwa Aprili 23, 2025, kwa ajili ya kupanga tarehe ya hukumu.
Katabazi ambaye anajitambulisha kuwa ni mdau wa mchezo wa soka na kocha wa mchezo huo mwenye leseni ya daraja C, iliyotolewa na TFF, alifungiwa na TFF kujishughulisha na masuala ya soko ndani na nje ya nchi maisha yake yote Mwaka 2021.
Alifungiwa baada ya kuliandikia BMT barua Juni 15, 2021 akilishtaki TFF kuwa limeshindwa kusimamia mchezo huo kulingana na Sheria, Kanuni na miongozo yake.
Kufuatia barua hiyo, aliitwa katika Kamati ya Maadili, lakini hakuhudhuria badala yake alijibu kuwa yeye si mwanachama wa Chama cha Makocha Tanzania (TAFCA) ambacho kiko chini ya usimamizi wa TFF, hivyo yeye si mwanachama wa TFF.
Juni 24, 2021 TFF lilichapisha katika tovuti yao, uamuzi wa kumfungia Katabazi maisha kujishughulisha na masuala ya soko ndani na nje ya nchi.
Hata hivyo, mwaka 2024 alifungua kesi Mahakama ya Kisutu dhidi ya TFF na wadhamini wake akipinga uamuzi huo wa kufungiwa.
Katika kesi hiyo ya madai namba 14708/2024, pamoja na mambo mengine alidai kuwa Kamati ya Maadili ya TFF haikuwa na mamlaka ya kutoa uamuzi huo dhidi yake kwa kuwa Kanuni za Maadili za TFF, Toleo la Mwaka 2021, zilizotumika kumfungia si halali.
Alidai kuwa kanuni hizo hazijasajiliwa na BMT kwa mujibu wa matakwa ya Sheria namba 12 ya mwaka 1967 na marekebisho yake na hivyo kuzifanya kuwa batili kutumika dhidi ya wanachama wake na mtu mwingine yeyote.
Katabazi alidai kuwa amri hiyo iliingilia haki yake ya kufanya kazi katika nyanja ya soka na hivyo kumkosesha fursa ya kupata mshahara na kipato kwa ajili ya kuendeleza maisha yake ya kila siku na familia yake, na kumsababishia maumivu ya kisaikolojia.
Hivyo aliiomba mahakama iiamuru TFF imlipe Sh600 milioni kama fidia ya madhara ya jumla aliyoyapata kutokana na uamuzi huo wa kumfungia maisha uliotolewa kwa makusudi, kimakosa na kwa nia ovu.
Pia aliomba alipwe Sh100 milioni kama fidia ya adhabu kwa kitendo cha wadaiwa kutoa uamuzi huo wakijua kuwa hawana mamlaka ya kisheria kuchukua hatua hiyo dhidi yake, riba ya kiwango cha Mahakama kwa tuzo (fedha ambazo ingeamriwa alipwe) na gharama za kesi.
Vilevile aliiomba mahakama itoe zuio la matumizi ya Sheria (Katiba) na Kanuni za Maadili za TFF, kwa madai kuwa si vyombo halali kwa kutokusajiliwa kwa utaratibu na unaofaa.
Miongoni mwa vielelezo alivyoviwasilisha mahakamani ni barua ya BMT ya Juni 13, 2022 iliyothibitisha kuwa yeye si mwanachama wa TFF.
Hata hivyo Mahakama ya Kisutu iliitupilia mbali kesi hiyo, kufuatia pingamizi la awali lililoibuliwa na TFF.
Katika uamuzi wake uliotolewa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Franco Kiswaga ilikubaliana na sababu ya pingamizi la TFF kuwa haikuwa na mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo. Hakimu Kiswaga alisema hakuna ubishi kwamba Katabazi ni mwanachama wa TFF.
Hivyo alikubaliana na wakili wa TFF, Rahim Shaban kwa mujibu wa Katiba ya TFF, mwanachama asiyeridhika na uamuzi wa Kamati ya Maadili anapaswa kukata rufaa katika Kamati ya Rufaa ya Maadili, lakini haukufuata utaratibu huo.
Hakimu Kiswaga alisema kwa Katiba ya TFF, TFF itakuwa na mamlaka kushughulikia migogoro yote ya soka ndani na mwanachama asiyeridhika, anaweza kupeleka shauri lake katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) baada ya kumaliza hatua zote ndani ya FFF.
Hivyo alisema mahakama hiyo haikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo kwani mlalamikaji, Katabazi alipaswa kukata rufaa Kamati ya Rufaa ya Maadili na kama asingeridhika angekata rufaa CAS kama Katiba ya TFF inavyoelekeza, ndipo akaifuta kesi hiyo.
Uamuzi huo ndio Katabazi alioukatia rufaa hii Mahakama Kuu, pamoja na sababu nyingine, akidai kuwa Mahakama ya Kisutu ilikosea kisheria kushughulikia pingamizi la wajibu rufani ambalo halikuwa na msingi wa kisheria na kwa kuzingatia ushahidi uliotolewa wakati wa usikilizwaji wa pingamizi.