Hukumu ya sheikh ponda yakumbwa na mizengwe leo

Hukumu ya sheikh ponda yakumbwa na mizengwe leo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
HUKUMU YA SHEIKH PONDA YAKUMBWA NA MIZENGWE LEO





HUKUMU ya Kesi inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya maandamano haramu imeahirishwa mpaka tarehe 9 mei mwaka huu.


Kesi hiyo imeharishwa baada ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Victoria Nongwa ,kutokuwepo Mahakamani hapo.

Awali hakimu huyo alitarajiwa kuketi katika kiti cha enzi na kutoa hukumu ya kesi hiyo Na.245/2012 inayomkabili Ponda na wenzake.

Aprili 3 mwaka huu:Mawakili wa upande wa Jamhuri ,Tumaini Kweka na Jessy Peter na mawakili wa utetezi Juma Nassor na Njama waliwasilisha majumuisho yao mahakamani hapo kwa njia ya maandishi ambapo mawakili wa upande wa jamhuri waliiomba mahakama iwaone washitakiwa wote wana hatia na wapewe adhabu kwa mujibu wa sheria.

Wakati mawakili wa utetezi waliiomba mahakama iwaone washitakiwa hawana hatia na iwaachilie huru kwa sababu hawakutenda makosa yanayowakabili na kwamba upande wa jamhuri umeshindwa kuthibitisha kesi yao.

chanzo.
HUKUMU YA SHEIKH PONDA YAKUMBWA NA MIZENGWE LEO - MPEKUZI
 
Back
Top Bottom