Hukumu ya uonevu yatolewa leo katika Mahakama ya Wilaya Karatu

Ni CC/99/2012. Mshtakiwa alishtakiwa kwa kosa la kulala na mwanafunzi wa sekondary, bila hata ushahidi wa kidaktari wala hata dada aliyekuwa rafiki wa mtuhumiwa kufika mahakamani kutoa ushahidi, kesi ikaingiliwa na DC, mtuhumiwa kafungwa miaka 30 leo.

Sheria inasemaje kwa kuwa hakukuwa na vipimo vya ki-daktari kuonesha kuwa kitendo hicho kilifanyika, pia shahidi muhimu ambaye ndiye dada anayesemekana kuwa alifanya kitendo hicho hakuitwa mahakamani kutoa ushahidi. Pia hakupimwa kuonesha manii hivyo kukosekana ushahidi muhimu (concrete evidence).

KUHUSIKA KWA MKUU WA WILAYA.

Mkuu wa wilaya bila ya kufanya utafiti kama wahusika walikuwa wapenzi ama la yeye alichosema ni kuwa madhali mtuhumiwa amekuwa na mahusiano na mwanafunzi afungwe miaka 30 na ndicho kilichofanyika leo.

Jina la mfungwa Emanuel Andrea. Kesi ilifunguliwa 29/09/2012.

Karatu haki kutendeka ni ndoto, kwani kesi nyingi ni za uonevu, ubabe na nguvu ya pesa.
 
Ni CC/99/2012. Mshtakiwa alishtakiwa kwa kosa la kulala na mwanafunzi wa sekondary, bila hata ushahidi wa kidaktari wala hata dada aliyekuwa rafiki wa mtuhumiwa kufika mahakamani kutoa ushahidi, kesi ikaingiliwa na DC, mtuhumiwa kafungwa miaka 30 leo.

Sheria inasemaje kwa kuwa hakukuwa na vipimo vya ki-daktari kuonesha kuwa kitendo hicho kilifanyika, pia shahidi muhimu ambaye ndiye dada anayesemekana kuwa alifanya kitendo hicho hakuitwa mahakamani kutoa ushahidi. Pia hakupimwa kuonesha manii hivyo kukosekana ushahidi muhimu (concrete evidence).

KUHUSIKA KWA MKUU WA WILAYA.

Mkuu wa wilaya bila ya kufanya utafiti kama wahusika walikuwa wapenzi ama la yeye alichosema ni kuwa madhali mtuhumiwa amekuwa na mahusiano na mwanafunzi afungwe miaka 30 na ndicho kilichofanyika leo.

Jina la mfungwa Emanuel Andrea. Kesi ilifunguliwa 29/09/2012.

Hii kesi inaweza kukatiwa rufani na mfungwa kuachiliwa.

Kama ni kweli ushahidi muhimu kama huo haukupelekwa mahakamani, hakuna kesi hapo. Inawezekana mshtakiwa hakuwa na mwanasheria wa kumsimamia, ndipo ikawa hivyo. Mtafutieni msaada wa kisheria, wapo wanasheria (TLS na NOLA) watakaotoa msaada wa kufungua rufani kwa niaba yake, bila gharama zozote.

Ni kesi rahisi.
 
Kule karatu wanaendekeza sana ngono wacha wajifunze. What if huyo binti angekuwa mwanao ungemtetea mshtakiwa?
 
Huyo DC ni yupi? Ni Kijiko au mwingine? Kweli Mahakama ya Karatu haitoi haki. Hatujui na Omar Kwaangw utendaji wake utakuwaje!
 
Kweli manoah hata mimi nilipopata taarifa hizi ilibidi niende eneo husika na nikapata taarifa kutoka ndani ya mahakama kuwa wameshinikizwa kutoa adhabu husika.

Msichana kahamishwa shule.
Kwa nini mahakimu wasiwajibishwe kwa hukumu ambazo haziendani na sharia?
 
Back
Top Bottom