Hukumu ya wanaodaiwa kuchoma Soko la Karume yasogezwa mbele hadi Agosti 2, 2024

Hukumu ya wanaodaiwa kuchoma Soko la Karume yasogezwa mbele hadi Agosti 2, 2024

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Hukumu iliyotakiwa kusomwa leo Julai 26, 2024 katika kesi ya jaribio la kuchoma soko la wafanyabiashara la Karume, Kesi Namba 313 ya Mwaka 2023 inayomkabili Christina Elisha na mwenzake Mashauri Ulomi imesogezwa mpaka Agosti 2, 2024.

Hukumu hiyo iliyotakiwa kusomwa na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Iala, Groly Nkwera imepangiwa Agosti 2 kwa kile kinachodaiwa kwamba mshtakiwa namba amelazwa katika moja ya hospitali Jijini Dar es Salaam.

Wakizungumza nje ya mahakama baadhi ya viongozi wa soko la Karume kwa nyakati tofauti waliwashauri Wafanyabiashara wenzao kuwa na subira katika kipindi hiki cha kusubiri hukumu ya Mahakama dhidi ya washtakiwa hao.

Geofrey Milonge, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara hao alisema ilikuwa isomwe hukumu, tunaiamini mahakama itatenda haki, Wafanyabiashara wawe watulivu kipindi hiki na kuhakikisha miundombinu ya soko letu inalindwa.

Milonge aliongeza kusema kwamba kwa uwingi wa Wafanyabiashara uliojitokeza mahakamani hapo ni ishara kwamba wapo wamoja kuliko wakati mwingine wowote
"Tupambane shauri hili lifike mwisho na iwe fundisho kwa wengine".

Naye, Mjumbe wa Kamati ya Soko la Karume, Athanas Mawala alisema kesi ni muda mrefu hivyo wangetamani vyombo vya habari viwasaidie kupaza sauti na hata hukumu ikitoka lakini itakuwa imeacha funzo kwa wengine wenye tabia ya kuchoma masoko kama ilivyotaka kujitokeza katika Soko Karume, Julai 6 2023.
 
Back
Top Bottom