Human brain vs computer

Dejong031

Member
Joined
Jun 7, 2020
Posts
92
Reaction score
96
Umeshawahi kujiuliza hivi ubongo wa binadamu na computer kipi kina uwezo Zaidi?, basi hili swali ni moja ya swali maarufu sana ambalo wanazuoni wengi wamekuwa wakijiuliza na kulifanyia utafiti, kwa miaka mingi.

Wengine wamejaribu kulimit comparison katika Nyanja nne ambazo ni ,
  • Energy efficiency
  • Storage
  • Memory
  • And processing speed.
  • Lakini leo tutaenda Zaidi ya hapo.
Umeshawahi kujipima uwezo wako wa akili na computer? Inawezekana jibu ni ndio, labda ulijaribu kujipa hesabu ndogo ili uone wewe na computer nani atatoa jibu haraka na computer ikakushinda, (hahaha), Ukichukua computer na ubongo wa bunadamu kwa haraka, utaona computer ni smart na inaspeed Zaidi ya ubongo, naam hii huifanya computer ionekane inauwezo Zaidi, lakini kuna mengi Zaidi nyuma ya stori hii, na ukweli ni kwamba ubongo wa binadamu unauwezo maradufu ya “ large contemporary super computer’’

Chukua porpcorn zako weka pozi zuri.

Kiwango cha nishati kinachoweza kukotolewa kutoka kwenye “fastest super computer” inayofanyakazi, kinaweza kutumika kuwasha jingo zima la kawaida, lakini ubongo unaweza kufanya kazi sawa na hiyo computer kwa kutumia nishati kidogo tu inayoweza kuwasha balbu inayofifia.

Kompyuta ya kawaida hutumia takriban wati 100 za nguvu. Ubongo wa binadamu, kwa upande mwingine, unahitaji takriban wati 10. Hivyo ni kweli, ubongo wako unatumia nishati mara kumi zaidi ya kompyuta. Ubongo unahitaji nguvu kidogo kuliko balbu.

Na tofauti kubwa ya kwanza kati ya ubongo na computer ni kwamba, ubongo unatumia glucose lakini computer inatumia umeme kwa upande wa nishati ( energy)

Makadirio hutofautiana kulingana na seli ngapi za neva, au niuroni, ziko katika ubongo wa kawaida. Tafiti nyingi zimekadiria ubongo unaweza kuwa na niuroni bilioni 100, wakati utafiti wa Chuo Kikuu cha Stanford unakadiria kuwa ubongo kweli una niuroni bilioni 200.

Unaweza kuwa unafikiria, "hapa utalinganisha vipi?, kompyuta ina byte na ubongo una niuroni. Tunawezaje kulinganisha hizi mbili?"

Twende sasa.

Tofauti moja kubwa kati ya ubongo wa binadamu na flash memory ya kompyuta ni uwezo wa niuroni kuchanganyikana yaani (storage na memory vimeungana). Kila neuroni ina takribani miunganisho elfu moja kwa niuroni zingine. Kwa miunganisho zaidi ya trilioni katika ubongo wa wastani wa binadamu, athari hii ya mwingiliano huunda uwezo mkubwa zaidi wa kuhifadhi.

Kulingana na uelewa wetu wa niuroni leo, ambao ni mdogo sana, tunaweza kukadiria uwezo wa kuhifadhi wa ubongo katika petabyte 1, ambayo inaweza kuwa sawa na zaidi ya SSD 1TB elfu, yaani kwa lugha nyingine GB million.

Tumalizie uzi huu, kwenye hii site hapa
HUMAN BRAIN VS COMPUTER
 
Sijui baadhi wanatumia nini kupembea mada hizi lakini niweke hili sawa ubongo wa binadamu huwezi kufananisha na kitu ambacho kishakuwa programed kufanya certain task not beyond of its scope
hata ubongo upo programmed pia
 
Haya ni mawasli wanayojiuliza watu wenye akili ama uwezo mdogo wa kufikiri.

Mtu mwenye akili timamu huwezi kuwaza swali kama hilo.
 
hiyo ni mada nyingine, lakini ukweli ni kwamba, bongo wetu pia upo programmed, ndio maana hakuna mtu anamfundisha mtoto kunyonya, au kumeza chakula.
Mkuu sitaki maelezo nani kauprogramm ubongo?
 
Bado ubongo wa Binadamu ni juu sana zaidi ya computer kiuwezo.

Kuna kipindi niliwahi kufanya maamuzi mawili kwa wakati mmoja kwa kasi kuliko hata mwanga unavyosafiri.

Nikiwa nimemuazima Rafiki yangu pikipiki nijifunze kuendesha, alinipatia kiroho safi, lakini muda huo ananikabidhi niliichukua kimihemuko bila kujua breki ni ipi sababu alipokaribia kusimama niliona aliachia klachi pikipiki ilisimama nami nilijua hiyo hiyo ndiyo breki.

Nilienda umbali wa 4 KM nikiachia klachi na pikipiki kupunguza mwendo nikijidanganya akilini kuwa hiyo ndiyo breki yake pikipiki hadi nilipogeuza na kurudi home.

Niliporudi salama nilisifiwa na marafiki kuwa nami ni miongoni mwao madereva wazuri wanaojua kuendesha pikipiki, hatimaye kichwa kikajaa sifa nyingi kupita kiasi na nilivuta mafuta ya kutosha kwenye pikipiki kuingia ndani ya fensi umbali wa mita 15.

Baada ya kuvuta sana mafuta na kuachia pikipiki iende na iliondoka kwa kasi kubwa sana, mbele kulikuwa na fensi ya sing'enge na nguzo ya umeme, cha ajabu akili ilinipatia ufumbuzi mara 2 baada ya kuona kila nilipoachia klachi pikipiki isimame nikidhani ni breki lakini haikusimama.

Akili ya kwanza ilikuwa kulazimisha kupita na pikipiki 1 kwa 1 kwenye fensi ila wakati huo huo hiyo akili ilinikataza kuwa nitaweza kufa, basi nilibadili maamuzi.

Akili ya pili iliniambia nikiona bado naenda mbele nilazimishe kuilaza pikipiki iserereke huenda ikaacha kuendelea na mwendo wa kasi iliyokuwa nayo ila akili hiyo hiyo ilinikatalia kuwa naweza kuvunjika miguu na kuchubuka vibaya sana, hatimaye akili ya pili ndiyo niliyofanya nayo maamuzi na kupona ingawa moshi wa pikipiki uliniunguza mkono baada ya kufanikiwa kulala na pikipiki chini huku matairi yakiwa yanazunguka, nikizidi kusifiwa na kujikuta huo moshi unaniunguza mkono wa kushoto lakini nilitoka mzima kabisa.

MASWALI:

Muda ulikuwa ni sekunde zisizozidi 2, lakini ubongo ulifanikiwa vipi kuchakata hizo akili zote 2 kwa wakati mmoja, kujadili na kufanya maamuzi sahihi kwa muda mchache tu huo wa sekunde 2?
 
Human brain ni zaidi ila speed na memory naipa computer lakini inategemea chip
 
Who programed our brains?
Compyuta bila kuwa na software(au program) haina kazi yoyote.... unapoiwekea program kama windows(unavyoiprogram) ndio inapata jina au identity kutokana na program ulioipa....utaskia mtu akisema "compyuta yangu ina edit video" mwingine "my gaming pc"..."windows pc" na kadhalika....

Anaye program ubongo ni "wewe".....bila "wewe" ubongo wako ni sawa na hardware. Yani wewe ndio program/software ya ubongo wako.
 
Umenielewa au umenijibu tu?
 
Swali gumu hili na ninafikiri binadamu hatutakuja kujua jibu , vipi unajua kabla hujazaliwa ulikuwa wapi? ukijibu hilo labda unaweza kupata jibu lako
Nimemuuliza huyu ambaye analeta mlinganyo usiowezekena anafananisha mtu na kitu alichokitengeneza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…