Humphrey Polepole na upinzani muko wapi?

Humphrey Polepole na upinzani muko wapi?

Patriot

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2008
Posts
5,705
Reaction score
4,703
Nilimtegemea kiongozi huyu mpenda kusema awe hewahi kuwaelekeza wenye uhitaji wa kugombea nafasi mbali mbali za majimbo ndani ya CCM wafanye nini. Naona yuko kimya baada ya mkutano mkuu. Nini kimempata? Au ni baada ya kugundua rushwa imetawala sasa yuko hoi?

Ninawategemea vyama vya upinzani pia waamke na kujinadi kwa nguvu maana bila hivyo, CCM itawalaza kwa kutosikika. Badala ya kutangaza kugombea Ubunge Mbowe, Mbatia, Zitto, nk. nilitegemea kusikia vyama vyao zaidi. Muko wapi ninyi wakati wenzenu wanatajwa kila kona? Au munajidai kuwa na mbinu za kisayansi! Sayansi gani hiyo?
 
Polepole kashavuta, upinzani wanakamatwa hata wakienda kuchukua form, nao wana watoto na familia zao. Toka na wewe ukachukue maana unajua kusoma na kuandika.
 
Wengi bado tunasikilizia kuna nini huko CCM. Bahati mbaya ni kama CCM imefungulia kila uchafu kuingia ndani. Hakuna taratibu, hakuna muelekeo, hakuna mwongozo. ni freestyle!
 
Back
Top Bottom