mtimawachi
JF-Expert Member
- Apr 1, 2020
- 2,108
- 3,155
Habari wanajamvi!
Nimemsikiliza kijana mwenzetu ndugu POLEPOLE katika hoja zake nyingi sana na mwisho hapa juzi akihojiwa.
IKANIBIDI nirudishe nyuma kumbukumbu hadi kipindi cha mchakato katiba mpya ulioongozwa na mzee wetu WARIOBA.
Katika ile tume,POLEPOLE alipewa ''airtime'' sana kupewa mialiko katika mijadala mbalimbali kuhusu rasimu ile.
Hata wanasiasa hasa chadema huyu alikuwa lulu kwao.
Nadhani hata kipenzi chetu MAGUFULI(RIP) alibaini kitu ndani yake akapenda kufanya nae kazi.
NINAAMINI kwa nafasi alizokuwa nazo kama ni fedha(mkwanja)anao na maisha tunayotamani wengi tayari ameshayavuka.
NIKAJIULIZA kama ndivyo nini kinamsumbua/kumuwasha kuzungumzia/kutetea hayo anayoyatetea? Kwanini asikae kimya tu aendelee na maisha yake? Mbona wenzake akina MAKONDA,BASHIRU nk wapo kimya?
LABDA nikiri wazi kwenye kipindi cha juzi katika wanahabari bora na makini kwa Tanzania yetu ni pamoja na yule kijana,lakini kwa kumwalika POLEPOLE nadhani hata yeye aliona kaingia kwenye msitu mwingine.
NIKIMAANISHA kilichoulizwa kilikuwa madini na kilichojibiwa madini.
Kuna usemi niliwahi usikia ''HERI YA KIJANA MDOGO MWENYE BUSARA KULIKO MFALME MZEE MPUMBAVU''
Katika tafakuri yangu nimebaini kuwa POLEPOLE ni kijana SHUJAA na MZALENDO wa kweli.
Na ndio maana anajitokeza hadharani kutoa mitizamo yake hata kama kuna watu wanaumizwa nayo.
ANA MAISHA maisha mazuri lakini kutokana na roho ya kizalendo alonayo anaona hivyo vyote si kitu ila awafungue na wengine bila kujali atafanywa nini.
KINGINE nimejiridhisha pasi na shaka kuwa CHADEMA hakifai kuwa mbadala wa CCM licha ya kuwa sasa NCHI inahitaji msaada wa mawazo mapya na chama kipya na sura mpya.
Namfananisha POLEPOLE na kijana mdogo mwenye busara.
Nawafanisha wale waliohudhuria kule kama wafalme wazee.
Wakati ni sasa vijana tuamke,hawa wazee wamefikia ukomo.
TUMUUNGE mkono POLEPOLE,tupinge kwa dhati matendo yanayoliangamiza taifa.(sio kupingapinga tu au kusifisifia tu.
NASIMAMA NA POLEPOLE.
NB:Kiitikadi mimi ni CCM tena timu MAGUFULI