Humphrey Polepole ni nani?

mwenye contact zake atuwekee hewani, huku kwetu tunaandaa mdaharo wa vijana kujitambua tunataka tumpe mada. Mwenye mawasiliano ayaweke kwenye inbox yangu
 
Ingia fb mtafute mwenewe au kuna best yake anaitwa juma mkuu utakuwa umempata
 
Ni kijana shupavu sana, na akisimama kuongea ndo mtu unatega sikio kusikiliza point, wengine vyama vyama vimewaziba macho na masikio
 


:third:

MKUU MPAKA SASA HUJAONA SABABU YA UKAWA KUTOKA NJE?, BADO HUJAJUA KWANINI TUME YA MZEE WARIOBA ILIVUNJWA HARAKA HARAKA???????????
 
mie mwenyewe nashangaa kina Mwesiga baregu kukaa kimya
Ni sahihi na busara kabisa Profesa Baregu kukaa kimya kwa sasa. Akiongea tutashindwa kujua anaongea kama mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Warioba au Kiongozi mwandamizi wa CHADEMA na sasa UKAWA.
 
jamaa ana element za kinyerere mimi nashauri tumbatize jina la MWALIMU NYERERE
 

Auaye kwa upanga atakufa kwa upanga.CCM wanajifanya nchi hii ni ya kwao na vitegemezi vyao.Mwisho wao uko karibu sana kuliko wanavyojidanganya. Wanatufanya WTZ ni wale wale wa miaka ile.Ole wao wataomba ardhi ipasuke.
 
mwenye contact zake atuwekee hewani, huku kwetu tunaandaa mdaharo wa vijana kujitambua tunataka tumpe mada. Mwenye mawasiliano ayaweke kwenye inbox yangu

Kweli vijana mna haki ya kujitambua na ni vizuri mkiwaalika mnaodhani wanaweza kuwasaidia kutokana na uwezo wao.Contacts zake ungeweza kuzipata kwenye tovuti ya kamati yao ila haipo hewani. Pengine zinaweza patikana kwenye utangulizi au hata mwisho wa kitabu chao cha rasimu ya mapendekezo ya wananchi kama utakipata.Au kusaidiwa na wadau wa jukwaa hili kwani wapo marafiki zake pia.
 
CCM hawajamchangachua? maana ukionekana ni virus kwao wanakumiliki kisaikolojia, kiuchumi, kimaisha, n.k
 
:third:

MKUU MPAKA SASA HUJAONA SABABU YA UKAWA KUTOKA NJE?, BADO HUJAJUA KWANINI TUME YA MZEE WARIOBA ILIVUNJWA HARAKA HARAKA???????????
usitake niwaze unachowaza na kufikiri wewe
 
Jamaa alikuwa ni mjumbe ktk tume ya warioba.Hakika dhamira aliyonayo na anavyoichambua rasimu utatambua tu wabunge wanajadili vitu ambavyo hawavielewi.

Ni dhahiri kwamba Ndugu H. Polepole ameonesha uwezo mkubwa katika kufikiri na kujenga hoja. Ingawa kwa wanaomfahamu wanasema ni mtu mwenye uwezo tangu akiwa shule na mahala pengine alikopita, lakini mimi naamini kwamba kuwepo kwake na kufanya kazi kwa karibu na kujifunza kutoka kwa watu kama Dkt Salim, Mzee Butiku, Mwenyekiti Warioba Jaji, Prof. Kabudi, Prof. Mwesiga, Marehemu Mvungi Dkt, Awadhi et al kumesaidia kumjenga sana na kuonekana hivi anavyoonekana mbele ya watanzania.

Siku zote mazingira ndiyo humbadilisha mtu. Huyu kijana nasema anabahati ambayo wengi hawana, na siku zote amshukuru MUNGU kwa hilo.

Hongera Humphrey.
 
Ni kati ya vijana wenye ujasiri ambao Tanzania iinapaswa kuwa nao. Hongera sana bwana polepole.
 
Nadahani ili kumfahamu mtu vizuri ni kupitia wasifu wake. Sasa ' ni noma maana yake nini?' Hapo ndiyo umelezea nini? Utakata kiu ya muuliza swali na wengine wengi wasiomfahamu Humphrey Polepoe?
Kile kichwa ni noma tulio soma Azania sec tunamfahamu vizuri sana!


selfish
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…